Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Katika Nchi Mbalimbali kwa Wakati Mmoja

    Kama yalivyokuwa matengenezo ya kame ya kumi na sita, harakati za Waadventista zilitokea katika nchi mbalimbali kwa wakati mmoja. Watu wenye imani walisoma unabii na wakaona ushahidi unaoonesha kuwa mwisho ulikuwa karibu. Kwa kusoma Biblia tu, makundi mbalimbali ya Wakristo, waliamini kuwa ujio wa Mwokozi ulikuwa umekaribia.TK 227.1

    Miaka mitatu baada ya Miller kufanya ufafanuzi wake wa unabii, Dr Joseph Wolff, “mmisionari kwa ulimwengu,” alianza kutangaza ujio wa Bwana uliokuwa karibu. Akiwa amezaliwa Ujerumani na wazazi wa Kiebrania, tangu alipokuwa kijana, alikuwa ameuamini ukweli wa dini ya Kikristo. Alikuwa msikilizaji mzuri wa maongezi katika nyumba ya baba yake wakati Waebrania waaminifu walipokusanyika kuelezea matumaini ya watu wao, utukufu wa Masihi aliyekuwa anakuja, na kurejeshwa kwa taifa la Israeli. Wakati mmoja, aliposikia Yesu wa Nazareti akitajwa, yule kijana alitakakujua, Yeye alikuwa nani. Jibu lilikuwa, “Myahudi mwenye vipaji vingi, ila kwa kuwa alijifanya Masihi, mahakama ya Kiyahudi ilimhukumu kifo.”TK 227.2

    Akazidi kuuliza swali jingine, “Ni kwa nini Yerusalemu imeharibiwa, na kwa nini tuko uhamishoni?” “Ahaa!” baba yake alijibu, “Kwa sababu Wayahudi waliwaua manabii.” Wazo likamjia pale pale: “huenda Yesu alikuwa nabii pia, na Wayahudi walimwua wakati hakuwa na hatia.” Ingawa alikuwa anakatazwa kuingia katika Kanisa la Wakristo, kijana huyu wa Kiyahudi alikuwa anakaa nje kusikiliza mahubiri. Alipokuwa na miaka saba tu, alikuwa anajivuna mbele ya jirani yao Mkristo juu ya ushindi ujao wa Israeli siku Masihi atakapokuja. Yule mzee alijibu kwa upole: “Kijana wangu mpendwa, ngoja nikwambie Masihi halisi alikuwa nani: Alikuwa Yesu wa Nazareti. ... ambaye babu zenu walimsulibisha. ... Nenda nyumbani ukasome Isaya 53, nawe utaamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.” 209Travels and Adventures of the Rev. Joseph Wolff, vol. 1, pp. 6, 7.TK 227.3

    Alikwenda nyumbani na kusoma Maandiko. Yalikuwa yametimia kikamilifu kabisa ndani ya Yesu wa Nazareti. Je, maneno ya yule Mkristo yalikuwa sahihi? Yule kijana alimwomba baba yake ufafanuzi wa ule unabii lakini alikutana na kimya kikali kiasi kwamba kijana hakuthubutu kuzungumzia tena jambo hilo.TK 228.1

    Akiwa na miaka kumi na moja tu, alikwenda ulimwenguni kutafuta elimu, kuchagua dini yake, na kazi yake katika maisha. Akiwa peke yake na bila pesa, ilimpasa kujitegemea. Alisoma kwa bidii, akijikimu kwa kufundisha Kiebrania. Aliongozwa kupokea imani ya Kanisa la Roma, naye akaenda kusoma katika Chuo cha Propaganda cha Roma. Hapa alikemea waziwazi maovu ya Kanisa na akataka kuwe na matengenezo. Baada ya Muda alifukuzwa. Ilikuwa wazi kuwa asingeweza kujisalimisha chini ya utumwa wa Kanisa la Roma. Alitangazwa kuwa jeuri na akaachwa aende ko kote alikokuwa anataka. Alikwenda Uingereza na kujiunga na Kanisa la Uingereza. Baada ya miaka miwili ya masomo, mwaka 1821 alianza kufuatilia lengo lake. Wolff aligundua kuwa unabii unadhihirisha ujio Wakristo kwa uweza na utukufu. Wakati akitaka kuwaelekeza watu wake kwa Yesu wa Nazareti kama Masihi aliyekuwa ameahidiwa, kuwaonesha ujio wake wa kwanza kama dhabihu ya dhambi, alikuwa akiwafundisha pia kuhusu ujio wake wa pili.TK 228.2

    Wolff aliamini kuwa ujio wa Bwana ulikuwa karibu. Fasili yake ya vipindi vya unabii iliuweka katika miaka ya karibu na kipindi kilichokuwa kimetajwa na Miller. “Je, Bwana wetu hakutupatia ishara za nyakati, ili tuweze kujua angalau kukaribia kwa ujio wake, kama mtu anavyojua kuwa majira ya joto yamekaribia kwa mtini kuchipua? Mambo ya kutosha yatajulikana kwa njia ya ishara za nyakati, kutufanya tujiandae kwa ajili ya ujio wake kama Nuhu alivyoandaa safina.” 210Joseph Wolff, Researches and Missionary Labors, pp. 404, 405.TK 228.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents