Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mauzo ya Vyeti vya Msamaha wa Dhambi

  Kanisa la Roma lilikuwa linaichuuza neema ya Mungu. Kwa kigezo cha kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Petro la Roma, mamlaka ya Papa ilikuwa inatoza na kuviuza vibali vya msamaha wa dhambi. Hekalu kwa ajili ya kumwabudu Mungu, lilijengwa kwa mapato ya udhalimu. Lilikuwa ni jambo hili lililowaamsha maadui wa uPapa waliofanikiwa na lililoongoza kwenye mapambano yaliyoitikisa enzi ya Papa na taji tatu juu ya kichwa chake.TK 82.3

  Afisa aliyeteuliwa kuuza vibali vya msamaha wa dhambi huko Ujerumani alikuwa anaitwa Tetzel. Ingawa alikuwa amethibitika juu ya uovu dhidi ya jamii na sheria ya Mungu; lakini aliajiriwa kuendeleza miradi yenye kumletea Papa fedha kutoka Ujerumani. Aliurudia-rudia uongo uliokuwa unang’aa na hadithi za kuvutia ili kuwadanganya watu wajinga na wenye mashaka. Endapo wangekuwa na Neno la Mungu, hawangedanganyika, lakini Biblia ilikuwa imezuiliwa wasiipate. 42See John C. L. Giesler, A Compendium of Ecclesiastical History, per. 4, sec. 1, Par. 5.TK 82.4

  Alipokuwa anaingia kwenye mji fulani, Tetzel alitanguliwa na mjumbe aliyekuwa anatangaza kuwa: “Neema ya Mungu na ya baba mtakatifu, ipo malangoni mwenu.” 43D’Aubigne, bk. 3, ch. 1. Watu walikuwa wanampokea mwigizaji huyu mwenye kukufuru; kana kwamba alikuwa Mungu mwenyewe. Tetzel, alipopanda mimbarani ndani ya kanisa, alikuwa anakisifia kibali cha msamaha wa dhambi kama ndiyo karama ya Mungu yenye thamani zaidi kuliko nyingine zote. Alitangaza kwamba tokana na ubora wa vyeti vyake vya msamaha; dhambi zote ambazo mnunuzi alikuwa anatamani kuzitenda baadaye, zingesamehewa na ” hata asingelazimika kufanya toba.” 44Ibid Aliwahakikishia wasikilizaji wake kuwa vyeti vyake vilikuwa na uwezo wa kumwokoa mtu aliyekufa; wakati ule-ule pesa inapogonga sakafu ya kasha la fedha, ile roho ambayo kwayo fedha hizo zilikuwa zimelipwa, ingeokoka kutoka toharani na kwenda mbinguni. 45See K. R. Hagenbach, History of the Reformation, vol. 1, p. 96.TK 83.1

  Dhahabu na fedha vilitiririka na kuingia ndani ya hazina ya Tetzel. Wokovu uliokuwa unanunuliwa kwa pesa ulikuwa unapatikana kwa urahisi zaidi ya ule uliokuwa unahitaji toba, imani, na jitihada za dhati kupingana na kuishinda dhambi. (Angalia Kiambatisho)TK 83.2

  Luther alikuwa amejawa na hofu. Wengi miongoni mwa kusanyiko lake, walikuwa wamenunua vyeti vya msamaha. Mara walianza kuja kwa Mchungaji wao, wakiungama dhambi na kutarajia kupata tamko rasmi kuwa wamesamehewa, siyo kwa sababu walikuwa na toba na walikuwa wanataka kufanya matengenezo, bali kwa misingi ya vyeti vya msamaha. Luther aliwakatalia na kuwaonya kuwa wasingefanya toba na matengenezo, wangeangamia pamoja na dhambi zao. Walimfuata Tetzel wakimlalamikia kuwa aliyekuwa anatakiwa kuwasamehe dhambi alikuwa amevikataa vyeti vyake, na baadhi walidai kwa ujasiri kuwa fedha zao zirejeshwe. Akiwa amejawa na hasira, mtawa huyo, alitamka laana za ajabu, akasababisha mtafaruku katika viwanja vya hadhara na alitangaza kuwa, “Alikuwa amepokea agizo kutoka kwa Papa kuwachoma moto waasi wote waliotarajia kupinga vyeti vyake vitakatifu sana vya msamaha” 46D’Aubigne, bk. 3, ch. 4.TK 83.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents