Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wajibu wa Kwanza wa Muhimu

  Haitoshi kuwa na dhamiri njema, kufanya kile mtu anachokifikiri kuwa ndio sahihi au kile mchungaji anachomwambia kuwa ni sahihi. Yampasa ayachunguze Maandiko yeye mwenyewe. Anayo chati inayoonesha kila alama ya barabarani katika safari ya kuelekea mbinguni, na hatakiwi kubahatisha katika lolote.TK 361.4

  Ni wajibu wa kwanza na wa muhimu wa kila kiumbe mwenye akili kujifunza kutoka katika Maandiko nini maana ya ukweli na kisha kutembea katika nuru na kuwatia moyo wengine kufuata mfano wake. Yatupasa tujihukumu sisi wenyewe kama ambavyo tutakavyojibu kwa ajili yetu mbele za Mungu.TK 361.5

  Wasomi, wakijifanya wenye hekima kubwa wanafundisha kwamba Maandiko yana siri, na kwamba yana maana ya kiroho isiyoweza kueleweka kutokana na lugha inayotumika. Watu hawa ni walimu wa uongo. Lugha ya Biblia yapasa ifundishwe sawasawa na maana yake ya kawaida, isipokuwa pale ambapo mfano au vielelezo vimetumika. Kama watu wangeisoma Biblia jinsi ilivyo ingefanyika kazi ambayo ingewaleta kwa zizi la Kristo maelfu kwa maelfu ambao kwa sasa wanapotea katika ukosefu.TK 361.6

  Maandiko ambayo wasomi wengi hawayaangalii kwa kina kana kwamba siyo ya muhimu yamejaa faraja kwa yule ambaye amejifunza katika shule ya Kristo. Uelewa wa ukweli wa Maandiko hautegemei sana uwezo wa akili katika kuyachunguza bali ni kuwa na kusudi moja, kuwa na shauku ya dhati ya kuipata haki.TK 362.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents