Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 20 - Kuupenda Ujio Wakristo

  Uamsho mkuu wa kidinr umetabiriwa katika ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14. Malaika anaonekana akiruka “katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa.” Akisema kwa sauti kuu, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufunuo 14:6, 7.TK 226.1

  Malaika anawakilisha umakini wa kazi inayopaswa kufanywa na ujumbe huo na nguvu na utukufu ambao utaambatana nayo. Kuruka kwa malaika “katikati ya mbingu,” ile “sauti kuu,” na kueneza kwa “kila taifa na kabila na lugha na jamaa” ni ushahidi wa kuenea kwa harakati hizo ulimwenguni kote kwa kasi. Jambo hii litakapotokea, litakuwa linatangaza mwanzo wa hukumu.TK 226.2

  Ujumbe huu ni sehemu ya Injili ambayo ingeweza kuhubiriwa katika siku za mwisho tu, kwani wakati huo saa ya hukumu itakuwa imekuja kweli. Danieli aliagizwa kuifunga na kuitia muhuri “hatawakati wa mwisho,“(Danieli 12:4.) sehemu ya unabii wake iliyokuwa inahusu siku za mwisho. Mpaka hapo ujumbe unaohusu hukumu usingeweza kuhubiriwa, kulingana na kutimia kwa unabii huu.TK 226.3

  Paulo alilionya kanisa lisitarajie kurudi kwa Kristo katika siku zake. Hatuwezi kutarajia ujio wa Bwana wetu kabla ya “ukengeufu” na utawala wa muda mrefu wa yule “mtu wa kuasi.” Tazama 2 Wathesalonike 2:3. Huyo “mtu wa kuasi”—ambaye pia ni “siri ya kuasi,” “mwana wa uharibifu,” na “yule asi,“—anawakilisha utawala wa Papa, ambao ungedumisha mamlaka yake kwa miaka 1260. Kipindi hicho kilikwisha mwaka 1798. Ujio Wakristo usingeweza kutokea kabla ya wakati huo. Tahadhari ya Paulo inajumuisha kipindi chote cha Ukristo hadi mwaka 1798. Baada ya ujumbe huo, ujio Wakristo ndipo utahubiriwa.TK 226.4

  Ujumbe wa namna hiyo haujawahi kuhubiriwa huko nyuma. Kama tulivyoona, Paulo hakuuhubiri, alionesha kuwa kuja kwa Kristo lilikuwa suala la baadaye sana. Wana matengenezo hawakuhubiri ujumbe huo. Martin Luther aliiweka hukumu kama miaka 300 hivi kutoka wakati wake. Lakini tangu mwaka 1798 kitabu cha Danieli kimefunuliwa, na wengi wamehubiri ujumbe wa hukumu iliyokaribia.TK 226.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents