Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wokovu wa Jumla Siyo Fundisho la Maandiko

  Wanaoamini juu ya wokovu wa jumla wanayapotosha Maandiko. Wanaodai kuwa watumishi Wakristo wanautangaza uongo uliotamkwa na nyoka pale Edeni kwa kurudia-rudia, “Hamtakufa hakika.” “siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu.” Anatamka kuwa mdhambi atiaye aibu - muuaji, mwizi, -mzinzi - baada ya kifo wataingia kwenye furaha kamili ya hali ya kutokufa. Uongo unaopendelewa kabisa, ulifaa kuupendeza moyo wenye tamaa ya mwili.TK 330.1

  Kama ingekuwa ni kweli kuwa katika saa ya mauti watu wote wanakwenda moja kwa moja mbinguni, huenda tungekitamani kifo badala ya uzima. Wengi wamekuwa wakiongozwa na fundisho hili kujiua. Baada ya kuchanganyikiwa na kuvunjika moyo, inaonekana kuwa ni rahisi kuukatisha uhai na kupaa hadi kwenye raha kamili ulimwengu wa milele.TK 330.2

  Ndani ya Neno lake, Mungu ametoa ushahidi wazi kuwa atawaadhibu wavunjaji wa sheria yake. Je, Yeye ana rehema kubwa mno kiasi cha kushindwa kumtendea haki mwenye dhambi? Uangalie msalaba wa Kalvari. Kifo cha Mwana wa Mungu kinashuhudia kuwa, “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23), ili kila uvunjaji wa sheria ya Mungu upate adhabu inayostahili. Kristo asiye na dhambi alikuwa dhambi kwa ajili ya mwanadamu. Aliibeba hatia ya dhambi na uso wa Baba yake ulikuwa umefichwa hadi moyo wake ulipovunjika na uhai wake kuangamizwa - haya yote ni kwa ajili ya kumwokoa mwenye dhambi. Na kila mwanadamu anayekataa kuupokea upatanisho uliopatikana kwa gharama kubwa kiasi hiki, ni lazima abebe mwenyewe hatia na adhabu ya dhambi.TK 330.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents