Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 27 - Uamsho Wa Kisasa Umefanikiwa Kwa Kiasi Gani?

    Mahali popote lilipohubiriwa Neno la Mungu kwa uaminifu matokeo yaliyofuatia yalithibitisha kuwa chanzo chake ni Mungu. Wenye dhambi waliyaona matokeo yake haraka. Hatia kuu ilizishika akili na mioyo yao. Walikuwa na ufahamu wa haki ya Mungu, na walilia, “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” Warumi 7:24. Kadiri msalaba ulivyofunuliwa, waliona kuwa ni kafara ya Kristo pekee ambayo ingewapatanisha kutokana na uasi wao. Kupitia damu ya Yesu walipata, “kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilizotangulia kufanywa.” Warumi 3:25.TK 286.1

    Watu hawa Waliamini na walibatizwa na wakasimama wakitembea kwenye upya wa uzima, kwa njia ya imani ya Mwana wa Mungu, kufuata nyayo zake, kuakisi tabia yake, na kujitakasa wenyewe kama na Yeye alivyo msafi. Mambo ambayo wakati fulani waliyachukia, sasa waliyapenda; na yale waliyoyapenda mwanzo, waliyachukia. Wenye majivuno wakawa wapole, wasiofaa na wenye kiburi wakawa makini na wasio na kimbelembele. Walevi wakawa watulivu, waasherati wakawa safi. Wakristo hawakutafuta, “kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi, bali... katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.” IPetro 3:3, 4.TK 286.2

    Uamsho ulikuwa na kawaida ya kutoa mwito mzito kwa wenye dhambi. Matokeo yalionekana katika mioyo ambayo haikunywea katika kujikana nafsi bali walifurahi kwa sababu walionekana wanastahili kuteseka kwa ajili ya Kristo. Wanadamu waliyaona mabadiliko ndani ya wale waliolikiri jina la Yesu. Hayo ndiyo matokeo ambayo miaka ya zamani yaliambatana na uamsho wa kidini.TK 286.3

    Lakini nafasi nyingi za uamsho siku hizi zinaonesha kinyume chake. Ni kweli kwamba wengi wanakiri kuongoka na kuna idadi kubwa ya watu wanaoongezeka makanisani. Pamoja na hayo matokeo, hayo si hakikisho kuwa kuna ukuaji katika maisha ya kiroho unaoambatana na ongezeko. Nuru inayong’aa kwa muda ghafla inazimika.TK 286.4

    Uamsho unaopendwa mara nyingi huchochea msisimko na kuamsha tamaa ya kufahamu mambo mapya na yale yenye utata. Waongofu wanaopatikana kwa njia hii wanayo shauku kidogo ya kusikiliza ukweli wa Biblia. Wanavutwa na huduma ya kidini yenye kitu fulani kinachosisimua.TK 287.1

    Kwa kila moyo ulioongoka kweli kweli, uhusiano wake na Mungu na mambo ya milele litakuwa ndilo somo kuu la maisha. Iko wapi ile roho ya kujitoa wakfu kwa Mungu katika makanisa maarufu ya siku hizi? Waongofu hawaachi majivuno na kuupenda ulimwengu. Hawako tayari tena kujikana nafsi na kumfuata Yesu aliye mpole na mnyenyekevu kama ilivyokuwa wakati wa kuongoka kwao. Utauwa umeondoka kwenye makanisa mengi.TK 287.2

    Pamoja na kutetereka kwa imani kulikoenea, wako wafuasi wa kweli Wakristo kwenye makanisa haya. Kabla ya kujiliwa na hukumu ya mwisho ya Mungu, kutakuwa na uamsho wa utauwa wa zamani miongoni mwa watu wa Bwana ambao haujashuhudiwa tangu wakati wa mitume. Roho wa Mungu atamwagwa. Wengi watajitenga kutoka kwenye makanisa ambayo kuupenda ulimwengu kumechukua nafasi ya upendo wa Mungu na Neno lake. Wachungaji wengi na watu wataukubali kwa furaha ule ukweli unaowaandaa watu kwa ajili ya kuja kwa Bwana.TK 287.3

    Adui wa roho anatamani kuizuia kazi hii, na kabla ya wakati wa harakati hizi kufika, atajitahidi kuzizuia kwa kuleta uamsho bandia. Ndani ya yale makanisa ambayo ataweza kuyaweka chini ya udhibiti wake, atafanya ionekane kuwa baraka ya pekee ya Mungu imemwagwa. Watu wengi watashangilia na kusema, “Mungu anafanya kazi ya kushangaza,” kumbe kazi ni ile ya roho mwingine. Kwa kutumia mfumo wa kidini, Shetani atajitahidi kuenezamvuto wake kwenye ulimwengu wa Kikristo. Kutakuwa na msisimko wa kihisia, kuchanganya ukweli na uongo, ambao utakuwa umeandaliwa vizuri ili kupotosha.TK 287.4

    Hata hivyo katika nuru ya Neno la Mungu si vigumu kutambua asili ya harakati hizo. Wakati wowote watu watakapoupuuza ushuhuda wa Biblia, kugeukia mbali na ukweli huu ulio wazi, ukweli unaoupima moyo na unaowataka kujikana nafsi na kuukana ulimwengu; hapo tutakuwa na uhakika kwamba baraka ya Mungu haijatolewa. Na kwa kanuni isemavyo, “Mtawatambua kwa matunda yao.” (Mathayo 7:12) ni ushahidi kwamba harakati hizi siyo kazi ya Roho wa Mungu.TK 287.5

    Ukweli wa Neno la Mungu ni ngao dhidi ya udanganyifu wa Shetani. Kuupuuzia ukweli huu umefungua mlango kwa maovu yaliyoenea sasa ulimwenguni. Kwa sehemu kubwa, umuhimu wa sheria ya Mungu hauonekani. Dhana potovu ya sheria ya Mungu imesababisha makosa kwenye uongofu na utakaso, ikishusha kiwango cha uchaji wa Mungu. Hapa ndipo inapopatikana siri ya ukosefu wa Roho wa Mungu kwenye uamsho wa siku zetu.TK 288.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents