Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mnyama na Sanamu Yake

  Yule mnyama mwenye pembe mbili “awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:16, 17. Malaika wa tatu anatoa onyo: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu.”TK 277.2

  “Mnyama” ambaye watu wanalazimishwa kumwabudu ni yule wa kwanza, au aliye mfano wa chui, yaani mnyama wa Ufunuo 13— mamlaka ya Papa. “Sanamu ya mnyama” inawakilisha ile aina ya uprotestanti ulioasi ambao utatokea makanisa ya Kiprotestanti yatakapotafuta msaada wa nguvu za dola kulazimisha kanuni zao. “Alama ya mnyama” bado inahitaji kufafanuliwa.TK 277.3

  Wale wazishikao sheria ya Mungu wako kinyume na wale wanaomsujudia mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake. Ushikaji wa sheria ya Mungu kwa upande mmoja na uvunjaji wa sheria hiyo kwa upande mwingine, utaweka tofauti kati ya wanaomsujudia Mungu na wale wanaomsujudia mnyama.TK 277.4

  Sifa bainifu ya mnyama na sanamu yake ni uvunjaji wa amri za Mungu. Danieli anasema hivi juu ya pembe ndogo, yaani mamlaka ya Papa: “Naye ataazimu kubadili majira na sheria.” Danieli 7:25. Paulo aliita mamlaka hiyo “mtu wa kuasi” (2 Wathesalonike 2:3), ambaye angejiinua nafsi yake juu ya Mungu. Mamlaka ya Papa ingeweza kujiinua nafsi yake juu ya Mungu kwa kubadili sheria ya Mungu tu. Kila atakayeishika sheria iliyobadilishwa hivyo huku akijua, atakuwa anatoa heshima kubwa mamlaka ya Papa, jambo ambalo ni ishara ya utii kwa Papa, badala ya Mungu.TK 277.5

  Mamlaka ya Papa ilijaribu kubadili sheria ya Mungu. Amri ya nne imebadilishwa ili kuruhusu uadhimishaji wa siku ya kwanza badala ya Sabato ya siku ya saba. Badiliko la makusudi linaelezewa hapa: “Naye ataazimu kubadili majira na sheria.” Badiliko la amri ya nne linatimiza unabii huu kwa usahihi kabisa. Hapa, mamlaka ya Papa inajiweka juu ya Mungu waziwazi kabisa.TK 278.1

  Wanaomwabudu Mungu watajulikana kwa namna wanavyoichukulia amri ya nne ambayo ni ishara ya uwezo wake wa kuumba. Wale wanaomwabudu mnyama watajulikana kwa juhudi zao za kuikanyaga kumbukumbu ya Mwumbaji na kutukuza jambo lililoanzishwa na Kanisa la Roma. Mamlaka ya Papa ilijigamba kwa mara ya kwanza kuhusu suala la Jumapili kuwa “siku ya Bwana.” (Angalia kiambatisho.) Lakini Biblia inaeleza kuwa siku ya saba ndiyo siku ya Bwana. Kristo alisema: “Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia.” Marko 2:28. Soma pia Isaya 58:13: Mathayo 5:17-19. Hoja inayotolewa kuWakristo alibadili Sabato inakanushwa na maneno yake mwenyewe.TK 278.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents