Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siku kuu ya Upatanisho

    Kuhani mkuu alikuwa anaingia patakatifu sana mara moja kwa mwaka, katika siku kuu ya upatanisho, kwa ajili ya kupatakasa patakatifu. Wana mbuzi wawili walikuwa wanaletwa na kupigiwa kura, “kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.” Walawi 16:8. Mbuzi wa BWANA alichinjwa kama sadaka ya dhambi za watu, na ilimpasa kuhani kuipeleka damu yake ndani ya pazia na kuinyunyizia mbele ya kiti cha rehema na pia kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba iliyokuwa mbele ya pazia.TK 261.5

    “Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.” Walawi 16:21, 22. Mbuzi wa Azazeli hakuwa anarudi tena katika kambi ya Israeli.TK 262.1

    Sherehe hiyo ilikusudiwa kuwafanya Waisraeli wahisi utakatifu wa Mungu na chuki yake dhidi ya dhambi. Kila mtu alikuwa anatakiwa kuitaabisha nafsi yake wakati kazi hii ya upatanisho inaendelea. Shughuli zote ziliwekwa kando, na ilikuwa inawapasa Israeli kuitumia siku hiyo kwa maombi, kufunga na kujihoji moyoni.TK 262.2

    Mbadala alikubalika badala ya mdhambi, ila dhambi ilikuwa haifutwi na ile damu ya yule mhanga: ilikuwa inahamishiwa patakatifu. Kwa kutoa hiyo damu, mwenye dhambi alikuwa anakiri mamlaka ya sheria, alikuwa anaungama makosa yake, na alikuwa anaonesha imani yake kwa Mwokozi aliyekuwa anakuja; lakini alikuwa haondolewi kabisa hukumu ya sheria. Siku ya upatanisho kuhani mkuu, baada ya kuchukua dhabihu kutoka katika kusanyiko, alikuwa anaingia patakatifu sana. Alikuwa ananyunyizia damu ya dhabihu hiyo kwenye kiti cha rehema, juu ya sheria, ili kutimiza matakwa ya sheria hiyo. Kisha akiwa kama mwombezi, alikuwa anazichukua dhambi hizo mwilini mwake na kuzipeleka nje ya patakatifu. Akiweka mikono yake juu ya yule mbuzi wa Azazeli, alizihamisha dhambi hizo kwa kielelezo toka kwake kwenda kwa yule mbuzi. Yule mbuzi alikuwa anakwenda nazo mbali, na kwa njia hiyo zilikuwa zinachukuliwa kuwa zimeondolewa kutoka kwa watu.TK 262.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents