Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Froment Mwalimu wa Shule

  Froment alianza kazi yake kama mwalimu. Ukweli aliokuwa amewafundisha watoto shuleni walikuwa wanausimulia nyumbani. Muda si mrefu wazazi walikuja kusikiliza mafundisho ya Biblia. Agano Jipya na vitini vilikuwa vinagawiwa bure. Baada ya muda, mtendakazi huyu pia alilazimishwa kukimbia, lakini ukweli aliokuwa anafundisha ulibakia kwenye vichwa vya watu. Matengenezo yalikuwa yameanzishwa. Wahubiri walirudi na hatimaye ibada ya Kiprotestanti ilianzishwa mjini Geneva.TK 149.4

  Mji ulikuwa umetangazwa kuwa na imani ya Matengenezo mara Calvin alipoyaingia malango yake. Alikuwa njiani kuelekea Bascl alipolazimishwa kupitia njia ya mzunguko iliyokuwa inapitia Geneva.TK 149.5

  Katika ziara yake hii, Farel alikuwa ameuona mkono wa Mungu. Ingawaje Geneva walikuwa wameipokea imani ya matengenezo, bado kazi ya kuwaongoa watu ni lazima ifanyike moyoni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na wala si kwa maagizo ya mabaraza. Ijapo watu wa Geneva walikuwa wamejitenga na mamlaka ya Roma, hawakuwa tayari kuachana na maovu yaliyokuwa yameshamiri chini ya utawala wake.TK 149.6

  Kwa jina la Mungu, Farel alimwapisha kwa dhati mwlnjilisti kijana kubaki na kufanya kazi hapo. Calvin alikuwa amerudi nyuma kwa hadhari. Alikuwa ameogopa kukutana na watu jasiri na wapenda machafuko wa Geneva. Alikuwa na hamu ya kupata mahali palipotulia kwa ajili ya kujifunza zaidi, na kutoka mahali pale, kwa njia ya machapisho, ayaelekeze na kuyaimarisha makanisa. Lakini hakudiriki kukataa. Ilikuwa imeonekana kwake “ya kuwa mkono wa Mungu ulikuwa umenyooshwa kutoka mbinguni na kumkamata, na kumzuia asitoke mahali ambapo alikuwa tayari kuondoka.” 148D’Aubigne, bk. 9, ch. 17.TK 150.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents