Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    29 — Yesu Aiokoa Sabato

    Sabato ilitukuzwa tangu kuumbwa kwa dunia. Kama jinsi ilivyowekwa kwa ajili ya watu, mwanzo wake ni “wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu waliposhangilia kwa furaha.” Ayubu 38:7. Nchi iliafikiana na mbingu.” Mungu aliona kila kitu alichoumba, na tazama ni chema sana.” Akastarehe siku ya furaha ya kumaliza kazi yake. Mwanzo 1:31.TVV 152.1

    Kwa kuwa Mungu alipumzika siku ya Sabato, aliitakasa, akaibariki.” Mwanzo 2:3. Akaitenga kwa ajili ya kutumika kwa mambo matakatifu. Ilikuwa ukumbusho wa kuumba, na ukumbusho wa uwezo wake, na upendo wake.TVV 152.2

    Vitu vyote viliumbwa na Mwana wa Mungu. “Vitu vyote vilifanywa naye; na pasipo yeye hakikuumbwa kitu chochote kilichoumbwa.” Yohana 1:3. Kwa kuwa Sabato ni ukumbusho wa uumbaji, hivyo ni ishara ya upendo wa uwezo wa Kristo.TVV 152.3

    Sabato huleta katika ushirika pamoja na Muumbaji. Katika nyimbo za ndege, katika kuhema kwa miti, na katika nyinbo za bahari, tunaweza kusikia sauti yake aliyenena na Adamu na Hawa katika Edeni. Nasi tunapoona uwezo wake ukionekana katika viumbe, tunapata farijiko, maana sauti iliyonena katika uumbaji na vitu vikaumbwa, ingali ikinena uhai katika roho zetu. “Aliyeamuru nuru kung’aa gizani, ili kutoa elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.”2 Wakorintho 4:6.TVV 152.4

    “Niangalieni wote, ncha zote za dunia mpate kuokoka, kwa maana ni Mimi Bwana, wala hakuna mwingine.” Isaya 45:22. Huu ni ujumbe ulioandikwa katika viumbe ambavyo Sabato iliwekwa kuwa ukumbusho wake. Wakati Bwana alipowaambia Waisraeli kutunza Sabato, alisema: “Nazo zitakuwa ishara kati yangu na ninyi, ili mjue kuwa mimi ni Bwana Mungu wenu.” Ezekiel 20:20.TVV 152.5

    Waisrael walijua Sabato kabla ya kufika Sinai. Njiani huko Sabato ilitunzwa. Sabato ilipovunjwa, Bwana alisema: “Mtakataa kushika sheria mpaka lini?” Kutoka 16:28. Sabato haikutolewa kwa ajili ya Waisraeli tu, bali kwa watu wote wa ulimwengu. Kama sheria yote ya amri kumi ilivyo, haibadiliki wala kufutika. Kristo alisema kuhusu sheria hiyo. “Mpaka mbingu na nchi zitakapopita, nukta moja ya torati haitapita.” Mathayo 5:18. Kwa hiyo kadiri mbingu na nchi zitakavyodumu, Sabato itaendelea kuwa ishara ya uwezo wa Mungu wa kuumba. Edeni itakapotokea tena duniani, Sabato, itatukuzwa na wote walioko chini ya jua, maana ni siku ya Mungu ya kupumzika. “Toka Sabato hata Sabato, wenye mwili wote watakuja kuabudu mbele za Bwana.” Isaya 66:23.TVV 153.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents