Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Dhamana ya Ufufuo Wetu

    Wakati sauti ya malaika mkuu iliposikika pale kaburini kuwa “Baba yako anakuita”, Mwokozi alitoka kaburini akiwa na uzima aliokuwa nao. Kristo alikuwa ametangaza kwa ushindi kwamba “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima.” Maneno haya yanatamkwa na Mungu peke yake. Viumbe wote walioumbwa hupata uzima kutoka kwa Mungu tu. Ni yeye aliye mamoja na Mungu ndiye awezaye kusema kwamba: Nautoa uzima wangu na kuutwaa tena. (Yohana 10: 18.)TVV 443.2

    Kristo alifufuka katika wafu kama malimbuko yao waliolala, na ufufuo ulitokea siku ile ile ambayo mganda ungeletwa mbele za kwa Bwana. Kwa muda wa miaka zaidi ya elfu moja, wakati watu walipokuwa wakienda Yerusalemu kwa Pasaka, mganda wa kwanza ulitolewa kama sadaka ya shukurani kwa Bwana. Mganda uliotolewa wakfu kwa Mungu uliwakilisha mavuno. Kwa hiyo ufufuo wa Kristo ni mfano na dhamana ya ufufuo wa wenye haki wote waliokufa. “Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.” (I Wathesalonike 4:14).TVV 443.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents