Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo avunja ukuta wa chuki

    Yesu alikuwa ameanza kuvunja kuta za chuki baina ya Wayahudi na watu wa mataifa, na kuhubiri Injili kwa ulimwengu wote. Alijichanganya kamili na Wasamaria, na kuwafanyia fadhili watu hawa waliodharauliwa. Alilala nyumbani mwao, akala pamoja nao, akafundisha katika njia zao, na akawatendea kwa wema kamiliTVV 102.3

    Katika hekalu la Yerusalemu katika ukuta mfupi uliotenganisha sehemu nyingine, palikuwapo na maandishi yakisema kwamba, hakuna mtu anayeruhusiwa kupita hapa isipokuwa Myahudi peke yake. Mtu wa mataifa kama angalipita sehemu hii, angalilipa maisha yake, yaani angaliuawa. Lakini Yesu asili ya hekalu hilo, aliwaletea watu wa mataifa wokovu walionyimwa na Wayahudi.TVV 102.4

    Wanafunzi walishangaa kwa vile Yesu alivyokuwa. Siku mbili walizokaa Samaria waaminifu kwake, walijizuia wasionyeshe hali ya ubaguzi, lakini mioyoni walikuwa na hali hiyo. Walikuwa wagumu kujifunza namna hiyo iliyowafanya wakose fadhili na huruma kwa watu. Lakini baada ya kupaa kwa Bwana, fundisho hili liliwajia kwa uwezo mpya. Walikumbuka hali bora ya Yesu, kuhusu usemi wake, fadhili zake, na jinsi alivyowahesabu watu waliodharauliwa. Petro alipokwenda kuhubiri Samaria alikuwa na roho ile ile. Yohana alipoitwa huko Efeso na Smirna, alikumbuka mambo ya Shekemu, na hali ya Bwana Yesu alivyokuwa.TVV 102.5

    Watu wanaojiita kuwa wafuasi wa Mwokozi, wanaweza kudharau na kutenga watu, lakini hakuna kutenga mtu kwa ajili ya mahali alikozaliwa, wala kabila, wala kitu chochote kisichomfanya mtu asimfadhili mtu, hata akiwa mwenye dhambi kiasi gani. Mwito wa injili hutolewa kwa wote katika kisima cha Yakobo Yesu, hakuacha kusema na mwanamke, ingawa alikuwa mwenye dhambi kiasi gani.TVV 103.1

    Kila mara alianza fundisho lake kwa watu wachache waliokuwa wakimzunguka, lakini watu waliopita njiani walizidi kuongezeka na kusikiliza, mpaka ukawa mkutano mkubwa ukawa ukimsikiliza Mwalimu wa mbinguni kwa mshangao mkubwa. Leo, anaweza kuwa na mtu mmoja tu, anamsikiliza mtenda kazi wa Bwana, lakini nani aweza kujua jinsi mvuto huo utakavyokwenda mbali?TVV 103.2

    Mwanamke wa Kisamaria alithibitisha jinsi alivyokuwa mtendakazi anayefaa, kuliko wanafunzi wa Yesu. Kwa njia ya mwanamke huyu, mji mzima uliletwa kwa Bwana. Kila mfuasi wa Bwana anayezaliwa upya ni mtendakazi. Anayekunywa maji ya uhai, huwa chemchemi ya kunywesha wengine, maji ya uzima. Anayepokea, huwa mtoaji. Neema ya Yesu inapokuwa moyoni mwa mtu, ni kama chemchemi jangwani, huwanywesha wote waliokuwa karibu kupotea, wapate burudiko la uzima.TVV 103.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents