Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mariamu alitii maongozi ya Roho Mtakatifu

  Mariamu hakufahamu umuhimu wa kitendo chake cha upendo. Hakuweza kueleza sababu ya kuchagua wakati ule kuwa wa kumtia Yesu mafuta. Roho Mtakatifu alikuwa amempangia naye amefuata maongozi yake. Uvuvio wa Roho hautoi sababu. Nguvu isiyoonekana, huusukuma moyo kutenda. Inayo sababu yake yenyewe. Mtu hutenda tu bila maelezo.TVV 313.3

  Kristo alimfafanulia Mariamu maana ya kitendo chake: “Kwa kuwa amenipaka mafuta, amefanya hivyo kwa ajili ya maziko yangu.” Kama vile kichupa cha marhamu kilivyovunjwa na kujaza nyumba kwa harufu nzuri, hivyo mwili wa Kristo ulikuwa uvunjwe lakini akitoka kaburini, ataijaza nchi yote na harufu yake nzuri. “Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato” Waefeso 5:2.TVV 313.4

  Kristo akasema: “Amini, nawaambia, kila ihubiriwapo Injili katika ulimwenguni wote na hili alilotenda, huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.” Mwokozi alisema kwa uhakika kuhusu injili itakavyohubiriwa ulimwenguni kote. Na kwa kadiri injili itakavyoenea ulimwenguni, tendo la Mariamu litaendelea kutoa harufu nzuri, na mioyo ya watu itaburudishwa kwa tendo lake hilo. Falme zitainuka na kuanguka na mashujaa watasahauliwa, lakini kitendo cha mwanamke huyu hakitafutika katika kumbukumbu za historia takatifu. Mpaka wakati utakapokoma, kichupa cha manukato kilichopasuliwa kitaendelea kueleza habari za upendo wa Mungu wa ajabu kwa wanadamu waliopotea.TVV 314.1

  Ni fundisho dhahiri kiasi gani Kristo angempatia Yuda! Yeye asomaye madhumuni ya kila moyo angeweza kufunua mbele ya waliohudhuria karamuni sura za siri katika maisha ya Yuda. Badala ya kuwahurumia maskini, alikuwa akiwaibia fedha zilizokusudiwa kuwasaidia. Lakini ikiwa Kristo angemuumbua Yuda, hili lingekazaniwa kama sababu ya kumsaliti. Hivyo Yuda angeweza kupata huruma, hata kutoka miongoni mwa wanafunzi. Mwokozi alijiepusha asimpe kisingizio cha usaliti wake.TVV 314.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents