Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uchungu wa Majuto ya Yuda

  Sasa Yuda akajitupa miguuni pa Yesu akimkiri kuwa Mwana wa Mungu, na akimsihi ajiondoe katika mikono ya watu hao. Mwokozi alijua kuwa Yuda hakuwa na majuto ya hakika, kwamba amemsaliti Mwana wa Mungu asiye na mawaa. Walakini hakusema neno lo lote la kumshutumu. Alimtazama Yuda kwa huruma, na kusema, kwa saa hii nalikuja ulimwenguni.TVV 406.4

  Kwa mshangao watu waliokusanyika pale waliona ustahimilivu wa Kristo kwa msaliti wake. Mtu huyu alikuwa ni zaidi ya mwanadamu. Lakini kwa nini hakujiokoa na kuwashinda watesi wake?TVV 406.5

  Maombi yake Yuda yakiwa kazi bure, Yuda alikimbia kwa haraka kutoka ukumbini akipiga kelele, Nimechelewa!. Alijisikia kuwa hawezi kuishi na kushuhudia Yesu akisulibiwa, na akiwa amekata tamaa alitoka nje na kwenda kujinyonga.TVV 406.6

  Baadaye siku hiyo, watu walipokuwa wanampeleka Yesu mahali pa kusulibishwa, waliiona maiti ya Yuda ikiwa chini ya mti mkavu. Uzito wake ulikuwa umekata kamba aliyotumia kujinyonga. Mbwa walikuwa wakiula mwili wake. Malipo yalionekana kuwa yanawapata watu wale waliokuwa na hatia ya damu ya Yesu.TVV 407.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents