Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hoja yenye nguvu zaidi

  Filipo hakumwambia Nathanaeli akubali ushahidi wa Mtu mwingine, ila amwone Kristo yeye mwenyewe. Njia moja muhimu ya kuongoa roho kwa Kristo, ni kudhihirisha tabia ya Kristo ndani yetu katika maisha yetu ya kila siku. Watu hupinga wengine wasikubali ujumbe kwa ajili ya tabia zisizo za Kikristo. Lakini maisha ya upendo bila kuwa ubinafsi, ndiyo hotuba yenye kuaminisha watu na kuwaleta kwa Kristo.TVV 72.2

  Neno la Mungu, likisemwa na mtu ambaye ametakaswa kwalo, huwa na uwezo wa kuleta uzima, na huingia katika roho za watu. Mtu akilipokea neno kwa upendo, atatamani kulieneza kwa wengine. Ataeneza kile ambacho amepata. Ushuhuda wake huwa kamili wa kuwaongoza wengine kwa Kristo.TVV 72.3

  Mtu anayetaka kuangaza nuru ya Yesu, lazima kwanza yeye mwenyewe awe nuru. “Anyweshaye, atanyweshwa mwenyewe.” Mithali 13:25. Ili kusudi tuingie furaha ya utukufu wa Kristo, yaani furaha ya kuona waliookoka kwa damu yake, inatulazimu tushirikiane naye katika kazi yake pia.TVV 72.4

  Ungamo la imani la Nathanael lilikuwa katika masikio ya Yesu sawa na wimbo mtamu: “Kwa sababu nilikuambia kuwa, nilikuona chini ya mti. Unaamini? Utaona mambo makuu kuliko haya.” Mwokozi alitazamia kazi yake ya kuhubiri habari njema za wokovu, akiwaganga waliovunjika, na kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao kutoka kwa Shetani. Yesu akaongeza tena, “Amin, amin nakuambia, tangu sasa utaona mbingu zikifunguka, malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”TVV 72.5

  Hapa Kristo alikuwa akisema kuwa, kando ya Yordani mbingu zilifunguka, Roho akashuka. Lakini ukaniamini, imani yako itaimarishwa. Utaona kuwa mbingu zimefunguka, wala hazitafungwa. Nimezifungua kwa ajili yako. Malaika wa Mungu wanashuka wakichukua maombi ya wahitaji na wenye dhiki kwa Baba, na kushuka kuleta tumaini, na shime, na uzima kwa wanadamu.TVV 72.6

  Wakati wote malaika hupitapita kutoka duniani kwenda mbinguni, na kutoka mbingum kwenda duniani. Kwa niia ya Kristo, na kwa njia ya watumishi wake huleta mibaraka ya Mungu kwetu. Mwokozi alipotwaa hali ya binadamu alichukua fadhaa zetu zote ambao ni wana wa Adamu Na kwa Uungu wake hutufikisha katika kiti cha Mungu.TVV 73.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents