Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yesu alifunua hali yao halisi mbele yao

    Maneno ya Yesu yalipiga kwenye shina la hali yao ya kujifanya kuwa wenye haki machoni pao wenyewe. Kila neno liliwakata kama kisu kikali kikatavyo, maana hali yao ya kujipa haki wenyewe ilifunuliwa wazi mbele yao. Sasa wakadharau imani ambayo ilielezwa na Yesu dhahiri. Hawakuweza kukubali kuwa mtoto aliyezaliwa katika hali ya nchi ya kimaskini, angaliweza kuwa Masihi, ila ni mtu wa kawaida tu. Wakashupaza mioyo yao wasiamini. Wakapiga makelele kwa hasira, wakimkataa Mwokozi. Ghadhabu yao ikaamsha kiburi chao cha kitaifa, na maneno yake yakazama katika makelele. Ghadhabu yao ikawaka wakawa tayari kuua.TVV 128.3

    Mkutano ukavurugika, wakamkamata Yesu, wakamtoa nje ya Sinagogi na kumtupa nje ya mji wao. Wakitaka kumwangamiza, walimtupa katika genge ili aanguke na kuangamia humo. Makelele yalijaa hewani. Wengine walikuwa wakimtupia mawe, wakati alipotoweka kwao kwa ghafla. Wajumbe wa mbinguni walikuwa pamoja naye katika fujo hizo, wakamtoa humo salama salmini.TVV 128.4

    Ndivyo ilivyo katika vizazi vyote, majeshi ya Shetani yako tayari kuwashambulia wafuasi waaminifu wa Kristo; lakini majeshi ya mbinguni huwazunguka wote wanaompenda Mungu na kuwakinga na fujo hizo. Katika umilele ndipo tutaelewa kuwa wajumbe wa mbinguni kutoka kwa Mungu walifuatana na sisi kila siku hatua kwa hatua.TVV 128.5

    Yesu hakuacha kuwatia watu watubu katika sinagogi. Karibu na mwisho wa kazi yake huko Galilaya, alikwenda tena katika kijiji cha kwao alikozaliwa. Sifa za mahubiri yake na miujiza yake, zilikuwa zimeenea katika nchi yote. Katika Nazareti sasa hakuna mtu ambaye hakukubali kuwa anao uwezo unaozidi wa kibinadamu. Kati yao kulikuwa na watu waliowaponya wagonjwa wao.TVV 129.1

    Sasa mara tena walipoyasikia maneno yake, watu wa Nazareti waliingiwa na Roho wa Mungu. Lakini hawakukubali habari za mtu huyu aliyezaliwa na kukulia hapa kwetu, na mkuu kuliko sisi. Kumbukumbu ya madai yake kuwa ni Masihi, ilikuwa inawakasirisha. Amesema kuwa wao kama Waisraeli wanapitwa na watu wa mataifa. Kwamba Mungu anawaona watu wa mataifa afadhali kuliko wao. Ingawa waliuliza kuwa, “Mtu huyu amepata hekima hii wapi na uwezo huu wa kutenda mambo makuu?’ Mathayo 13:54, walikuwa hawako tayari kumkubali kama Kristo Mwana wa Mungu. Kwa sababu, ya kutoamini kwao, Kristo hakufanya miujiza mingi huko kwao, na zaidi aliondoka kwao, wala hakurudi tena.TVV 129.2

    Kutokuamini kulikoshikiliwa na watu wa Nazareti, kuliendelea hata katika Sanhedrini, na taifa lote likawa katika hali hiyo. Hali hiyo iliongoza mpaka kwenye msalaba wa Kalwari, na mpaka kuharibiwa kwa mji wao, mpaka kutawanywa kwa taifa lao katika mataifa ya kishenzi.TVV 129.3

    Kristo alitamani kuwafunulia Waisraeli hazina za ukweli wenye thamani. Lakini wao waling’ang’ania mambo yao yasiyofaa, na maadhimisho yao ya dini bandia. Walitumia fedha zao kununua makapi na takataka tu, wakati mkate wa uzima ulikuwako. Kristo alitaja mara nyingi mambo ya unabii, na kusema; “Maneno haya leo yametimia masikioni mwenu.” Kama wangelichunguza maandiko kwa makini, wakilinganisha mambo yao na Neno la Mungu, Yesu asingelikuwa na sababu ya kusema: “Angalieni nyumba yenu imeachwa ukiwa.” Luka 13:35. Ajali iliyowaangukia na kuuteketeza mji wao, ingeliepukwa, kama wangejali maonyo.TVV 129.4

    Lakini mafundisho ya Kristo yaliyotaka watu Watubu hayakufuatwa. Kama wangefuata mafundisho yake, mambo yao lazima yangegeuka, na matumaini yangekuja wima. Lazima waende kinyume na wataalamu wao na walimu wao.TVV 129.5

    Viongozi wa Wayahudi walikuwa na kiburi na majivuno. Walipenda kuketi katika viti vya mbele ndani ya masinagogi. Walipenda kutajwatajwa kwa majina ya heshima na watu. Na kama hawakuheshimiwa hivyo walikuwa wachungu wenye wivu. Mawazo yao yakawa giza tupu kwa ajili ya ubinafsi, na chuki, wala hawakuweza kupatanisha hali yao na uwezo wa Kristo mwenye kuongoa na maisha yake matakatifu. Maisha ya Kristo ya kimaskini hayakuafikiana na madai yake ya kuwa Masihi. Mbona anajifanya namna hii? Kama ndivyo anavyodai kuwa Masihi, mbona hana jeshi lenye silaha? Anawezaje kuwokoa Wayahudi kwa njia hii?TVV 129.6

    Lakini Wayahudi hawakumkataa kwa ajili ya kutokuwa na mambo hayo, ila walimkataa kwa kuwa alikuwa kikwazo kwao kwa ajili ya maisha yake matakatifu, na maisha yao ni machafu. Utawa wake ulifunua hali yao ya uchafu, wakaonekana jinsi tabia zao zilivyo chafu. Nuru kama hiyo haikutakiwa kabisa. Wangeishi na hali hiyo ya uchafu, kuliko kuwa na hali Safi ya Yesu inayodhihirisha aibu yao. Wala hawakutaka hata kuwa mbele yake.TVV 130.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents