Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Usikose kuongea na Mungu kwa sababu ya shughuli nyingi mno

    Hakuna mtu aliyekuwa na kazi nyingi maishani kama Yesu; walakini alikutwa akiomba mara ngapi! Mara kwa mara imesemwa kwake hivi: “. . . akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.” “Lakini habari zake .... Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.” “Ikawa siku zile aliondoka alienda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu,” Marko 1:35; Luka 5:15, 16; 6:12.TVV 200.2

    Mwokozi aliona kuwa ni lazima aache shughuli za maisha na kujitenga kwa maombi; ili kiungo kinachowaunganisha na Baba yake kisivunjike. Kama mmoja wetu, alikuwa akimtegemea Mungu kamili. Katika sala za siri alitafuta uwezo wa Uungu ili apate kufanya kazi yake akiwa na silaha na nguvu za kutendea mambo.TVV 200.3

    Yesu alivumilia uchungu wa maisha na matizo yake. Katika kushirikiana na Mungu aliweza kuvumilia mzigo wa dhambi uliomlemea. Yesu kama binadamu alikabiliana na kiti cha enzi cha enzi cha Baba, mpaka akapta moto upya, kama betri ya gari. Hiyo ilimvunganisha binadamu na Mungu ikamwezesha. Alipokea uzima kutoka kwa Mungu ili apate kuutoa uzima huuo ulimwenguni. Hali yake hiyo lazima iwe yetu.TVV 200.4

    Leo kama tungepata wakati wa kwenda kwa Yesu na kumweleza mahitaji yetu, angetutimizia. Yeye ni Mshauri wa Ajabu. Tunaambiwa kumwomba hekima, huwapa watu wote kwa ukarimu, wala hazuii. Isaya 9:6; Yakobo 1:5TVV 200.5

    Kila mtu anahitaji apate ujuzi kamili wa kumjua Mungu; na mapenzi yake. Lazima tumsikie akisema, sisi binafsi, sauti zote zikinyamaza, lazima tumsikie akituzungumzia mioyoni mwetu. Tunaponya-mazisha sauti zote, ndipo tunapoweza kuisikia sauti ya Mungu akinena nasi. Zaburi 46:10. Hapa ndipo pumziko la hakika linaweza kupataikana. Mtu anayepumzika kwa jinsi hii ndiye atakuwa na uwezo na nguvu za kuwaongoa wanadamu wenzake.TVV 201.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents