Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kujidanganya kwa ubinafsi

    Chachu hufanya kazi yake bila kuonekana, ikichachua chakula kwa jinsi yake. Vivyo hivyo hali ya unafiki ikikubalika huchachua tabia na kuharibu mtu. Waandishi na mafarisayo walifunika hali halisi ya mafundisho ya Biblia, wakatia polepole mambo mengine na kuyatia katika nia zao. Mfumo huu wa udanganyifu husababisha ugumu wa kuamini mameno ya Kristo.TVV 229.1

    Hali hiyo hiyo huwadanganya watu wale wanaojaribu kuitafsiri sheria ya Mungu ifuate mawazo yao, na matendo yao. Watu hawa hawaishambulii sheria ya Mungu waziwazi, ila hufiriri mawazo yaliyo ya hatari kuwa kama kanuni ya hali yao. Hueleza hivyo ili kuharibu maana yake.TVV 229.2

    Unafiki wa Mafarisayo ulikuwa matokeo ya kujitafutia ubwana. Hivyo waliongozwa kupotosha Maandiko Matakatifu. Uovu huu wa kijanja hata wanafunzi pia waliupendelea. Wafuasi wa Yesu, kwa sehemu kubwa walivutwa na madhumuni ya Mafarisayo, kuhusu kuamini au kutoakuamini. Hata wanafunzi pia walikuwa wakipenda kujitafutia umaarufu. Roho ya namna hii ilisabaabisha mashindano, kwamba, ni nani atakuwa mkuu zaidi. Jambo hili liliwafanya kuwa wadogo sana machoni pa Kristo ambaye ni mwenye maisha ya kuinyima. Jinsi chachu ilivyoharibu, ndivyo hivyo, kujitafutia umaarufu, kunapopendelewa, huchafua, na kuharibu mtu.TVV 229.3

    Leo, kama ilivyokuwa zamani, dhambi hii ya kujitakia ukubwa, imeenea kiasi gani! Watu wao tayari kiasi gani kuandamia hali ya kutaka umaarufu na upendeleo wa watu! Upendo wa ubinafsi, kutamani anasa na kupingana na kusudi la Mungu, na njia alizoweka, mambo hayo husababisha kuhafifisha neno la Mungu na kutukuza mawazo ya binadamu zaidi ya mpango wa Mungu.TVV 229.4

    Dini ya Kristo ndiyo inayoelekezwa na Roho Mtakatifu, uwezo wa Mungu peke yake ndio unaoweza kuondoa ubaya wote, na unafiki. Badiliko hili huja kwa mtu kwa ajili ya kazi yake, yaani kwa njia ya Roho wake Mtakatifu, wakati imani tunayoamini inapokuwa ya hakika, haharibu upendo wa ubinafsi na kujipendekeza ambako si kweli. Hivyo sisi hutafuta utukufu wa Mungu, wala sio mapenzi yetu. Hali hiyo ikitokea tunaweza kujua kuwa tuko katika njia ya kweli. Kusudi la Kristo lilikuwa, “Baba, ulitukuze jina lako ...” Yohana 12:28. Na sisi tunapomfuata Yeye, hili Utakuwa kusudi letu pia.TVV 229.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents