Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yesu Atokwa Na Machozi

  Yesu alilikazia macho tamasha, na umati ukawa kimya, wakiwa wamepigwa na butwaa kwa uzuri. Macho yote yalielekezwa kwa Mwokozi’ Wakashangazwa na kuhuzunishwa kuyaona macho yake yakilengwalengwa na machozi huku mwili wake ukisukasuka kama mti uliokumbwa na kimbunga. Kilio cha uchungu kilisikika ghafla kutoka katika midomo yake iliyokuwa inatetemeka, kama vile kutoka katika moyo uliovunjika. Ni shani ya jinsi gani kutazamwa na malaika! Ni shani ya jinsi gani kuangaliwa na makutano yenye furaha yaliyokuwa yanamsindikiza kuingia mji mtakatifu, ambapo walitegemea alikuwa karibu kutawala! Huzuni hii ya ghafula ilikuwa kama ishara ya kilio katika jamii inayoshangilia. Mfalme wa Israeli alikuwa analia; siyo machozi ya furaha ya kimya, bali ya uchungu usiozuilika. Kwa ghafla makutano wakapigwa na giza la huzuni. Wengi wakilia kwa huruma na huzuni wasiyoweza kuielewa.TVV 322.2

  Mbele ya Yesu kulikuwa Gethsemane, ambako muda si kitambo giza kuu la kutisha litamkabili. Lango la Kondoo pia lilikuwa likionekana, ambalo ndio kondoo wa kafara walipokuwa wakipitia kupelekwa machinjoni. Lango hii karibu lifunguliwe ili Yeye aingie ambaye ndiye Kondoo wa kafara wa kweli, na ambaye kondoo waliochinjwa walikuwa mfano wake. Karibu hapo kulikuwa na Kalwari, mahali hasa pa uchungu uliokuwa unamkaribia. Walakini huzuni yake siyo ya ubinafsi. Wazo la huzuni ya nafsi yake halikutisha roho yake. Kitu kilichomhuzunisha ni kule kuuona mji wa Yerusalemu, Yerusalemu uliokuwa umemkataa Mwana wa Mungu, na kuudhihaki upendo wake, na ulikuwa unapanga kumwua. Aliona jinsi ambavyo ungekuwa ikiwa ungemkubali yeye pekee ambaye angeuponya jeraha lake. Angewezaje kuuachilia mbali?TVV 322.3

  Waisraeli walikuwa watu waliopendelewa sana; Mungu alikuwa amelifanya hekalu lake kuwa makazi yake; “Kuinuka kwake ni mzuri sana, ni furaha ya dunia yote.” Zaburi 48:2. Kwake Yehova ameonyesha utukufu wake, makuhani wamehudumu, kawaida za dini na ibada zimefanyika miaka yote. Lakini haya yote lazima yakome. Yesu alipunga mkono wake juu ya mji ulikuwa unaijiliwa na ajali, na kwa huzuni alisema: “Laiti ungejua, hata wewe, katika siku hii yapasayo amani yako! “Mwokozi hakuyasema mambo jinsi yangelikuwa kama wangalitafuta msaada wa Mungu, na shukrani yao kwake kwa kumtoa Mwanawe kama zawadi. Yerusalemu ungalisimama katika majivuno ya mataifa na falme kwa msaada wa Mungu, wala Warumi wasingalikanyaga ndani yake. Mji ungalidumu kati ya miji mikuu ya dunia.TVV 322.4

  Mwokozi aliacha kusema vile ambavyo hali ya Yerusalemu ingekuwa kama ungekuwa umekubali msaada ambao Mungu alitamani kuupatia tuzo la Mwana wake. Yerusalemu ungeendelea kutukuka kama fahari ya usitawi, malkia katika madola, ukiwa huru katika nguvu za enzi itokanayo na Mungu, na bendera za Warumi kamwe zisingepepea juu ya kula zake. Mwana wa Mungu aliona kuwa ungekuwa huru kutokana na utumwa na kusimamishwa kama mji mkuu wa dunia. Kutoka katika kuta zake njiwa wa amani mngeruka kuyaendea mataifa yote. Ungekuwa taji ya utukufu wa ulimwengu.TVV 323.1

  Lakini Mwokozi alijua kuwa sasa Yerusalemu uko chini ya utawala wa Warumi, ukikabiliwa na adhabu ya Mungu kama malipo yake, ila sasa mambo haya yamefichika kutoka machoni mwake. “Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakuzingira na kukujengea maboma, kukuzunguka, nao watakubomoa kabisa, hata mawe ya msingi wake yatafukuliwa kabisa, jiwe lisibaki juu ya jiwe jingine kwa sababu hukujua majira ya kujiliwa kwako.”TVV 323.2

  Yesu aliona mji wenye ajali, ukizingirwa na adui zake hata kuangamia kwa njaa na kwa upanga, mama wakila mizoga ya watoto wao, na wazazi wakinyang’anyana mizoga ya waliokufa kati yao wao kwa wao. Upendo wa mama kwa watoto wao utatoweka kabisa kwa sababu ya njaa. Yesu aliona kuwa ugumu wa Wayahudi utawafanya wasisalimu amri kwa washambuliaji wao na hivyo wajivutie mateso bila sababu. Aliona misalaba ikiwekwa na watu wakiangikwa juu yao. Aliona jinsi majumba mazuri ya kifalme yatakavyoharibiwa, na hekalu lao wanalojivunia aliliona katika hali ya maangamizo yasiyosemekana, na katika kuta zake kuu hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe jingine ambalo halikubomolewa. Aliona mji mashuhuri ukilimwa kama shamba.TVV 323.3

  Jinsi baba anavyomwombolezea mtoto wake, aliyekufa, ndivyo Yesu alivyouombolezea mji wa Yerusalemu. Alisema: “Nitawezaje kukuacha? Nitawezaje kukuona ukiwa ndani ya magofu? Jinsi jua litakavyopita juu yako likienda kutua upande wa magharibi, ndivyo Yerusalemu utakavyokoma.” Wakati maandamano yalipokuwa yangali yakisimama penye mlima wa mizeituni nafasi ya kuokoka: kwa Yerusalemu ilikuwa bado iko.TVV 324.1

  Wakati mishale yajua ilipokuwa ikizama taratibu, upande wa magharibi, malaika hawawezi kuwatubisha watu hawa wapate kuuona upendo wa Mwokozi? Mji mzuri usio, mtakatifu uliowaua manabii na kuukataa upendo wa Mwokozi, siku yake ya mwisho ilikuwa inafikia mwisho, yaani mwisho wa rehema.TVV 324.2

  Hata hivyo Roho wa Mungu atasema na watu wa Yerusalemu tena. Kabla ya mwisho wa siku ushuhuda mwingine wa Yesu utatolewa. Kama Yerusalemu ungalimpokea Mwokozi alipoingia kwake kwa shangwe, ingeweza kuokolewa.TVV 324.3

  Lakini wakuu wa Yerusalemu hawakumtaka Mwana wa Mungu. Maandamano yalipokuwa karibu kupanda katika kilima cha mizeituni wakuu walizuia njia wakiuliza kuwa sababu ya ghasia hiyo ni nini? Walipouliza kuwa “Huyu ni nani?” Wanafunzi wakijaa na roho ya ujasiri, walikariri unabii unaomhusu Kristo.TVV 324.4

  Adamu atawaelezeni. Huu ni uzao wa mwanamke utakaoponda kichwa cha nyoka. (Tazama Mwanzo 3:15). Ibrahimu atawaambia: Ni Melkizedeki, Mfalme wa Salemu, Mfalme wa Amani. (Tazama Mwanzo 14:18) Yakobo atawambia: Ndiye Shilo wa kabila la Yuda, Isaya atawaelezeni, “Imanueli, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.” Isaya 7:,14; 9:6.TVV 324.5

  Yeremia atawaelezeni “Shina la Daudi. Bwana ni Haki yetu.” Yer 23:6. Danieli atawaelezeni: “Yeye ni Masihi (Mtiwa mafuta).” (Tazama Dan 9:24-27). Yohana Mbatizaji atawaeleza: “Yeye ni Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana 1:29.TVV 324.6

  Yehova Mkuu ametangaza: “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu.” Mathayo 3:17. Sisi wanafunzi wake tunatangaza: “Huyu ni Yesu, Masihi, Mkuu wa uzima, Mkombozi wa ulimwengu.”TVV 324.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents