Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uovu ulifunuliwa

  Mwujiza huu zaidi ya mingine, kwa Petro yalikuwa maonyesho dhahiri ya uwezo wa Mungu. Ndani, ya Yesu aliona uwezo wote wa kutawala mambo yote. Aibu ikampata kwa kutokuamini kwake. Shukrani kwa wema wa Yesu, zaidi ya yote, akijiona kuwa yu mwenye dhambi akiwa mbele ya Mungu aliye mtakatifu, akashangaa sana. Akaanguka miguuni mwa Mwokozi akilia: “Ondoka kwangu, maana mimi ni mwenye dhambi Bwana.”TVV 132.3

  Hali hiyo hiyo ya kuwa mbele ya utakatifu, ndiyo iliyompata nabii Danieli, alipoanguka mbele ya malaika akawa kama mfu. Soma Danieli 10:8. Isaya naye alilia: “Ole wangu kwani nimepotea, kwa kuwa mimi ni mwenye midomo michafu . . . kwa kuwa macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi.” Isaya 6:5. Hivyo imekuwa hali hiyo kwa wote waliopata kuuona utukufu wa Mungu.TVV 132.4

  Mwokozi alimjia Petro akasema: “Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.” Baada ya Isaya kuona, utakatifu wa Mungu, na kujiona jinsi asivyofaa yeye mwenyewe, alikabidhiwa ujumbe wa mbinguni ili autangaze, Baada ya Petro kuona kuwa mwenye dhambi, asiyefaa kitu, alipata mwito wa kufanya kazi ya Kristo.TVV 132.5

  Wanafunzi walikuwa wameona miujiza mingi ya Kristo, na walikuwa wamesikiliza mafundisho mengi ya Kristo pia, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa ameacha mambo yake, au shughuli zake za kwanza. Kifungo cha Yohana Mbatizaji kimekuwa cha kusikitisha sana. Kama hayo ndiyo matokeo ya kazi ya Yohana, walikuwa na matumaini madogo sana kwa Bwana wao, na kwa vile waongozi wa dini walivyokuwa wakimpinga. Kwao ilikuwa nafuu kurudi katika kazi zao za uvuvi kwanza. Lakini sasa Yesu anawaita waache mambo yao ya zamani, na washrikiane naye kazini. Petro alikuwa amekubali. Walipofika pwani, Yesu aliwaambia wengine watatu: “Nifuateni, nami nitawafanya wavuvi wa watu.’ Mara wakaacha vyote wakamfuata.TVV 133.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents