Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Karne za giza za mateso

    Kutoka katika maangamizi ya Yerusalemu Kristo aliunganisha habari na historia inayomalizia mwisho wa ulimwengu, kurudi kwa Mwana wa Mungu katika nguvu na utukufu. Kati ya matukio mawili haya kutakuwa na karne nyingi za giza kuu, karne ambazo kanisa lake takumbwa na umwagaji wa damu, huzuni na mateso. Yesu alipitia matukio haya kwa muhtasari tu. “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea nanma yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.TVV 355.3

    Kwa muda zaidi ya miaka elfu moja wafuasi wa Kristo watapata mateso ambayo ulimwengu haujayaona. Mamilioni ya wafuasi wake waaminifu watauawa. Kama mkono wa Mungu usingalinyoshwa ili kuwalinda watu wake, wote wangalipotea kabisa.TVV 355.4

    Sasa, Bwana akazungumzia kurudi kwake kwa usemi wa wazi “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki. Kwa maama watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” Katika mikutano ya maelfu wanaodai kuongea na wafu, je hapasikiki wito wa, “Tazama, Kristo yumo nyumbani?” Haya ndiyo madai yanayofanywa na roho za mizimu. Lakini Kristo anasemaje? “Msisadiki”TVV 355.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents