Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Faida ya ajabu ya Maombi

    Mwokozi alieleza siri ya kufaulu kwao itakuwa katika kuomba uwezo na neema katika jina lake. Maombi ya mtu mnyenyekevu Kristo atayawakilisha mbele za Baba kama yake mwenyewe kwa niaba ya mwombaji. Sala ya unyofu yawezekana isiwe yenye maneno ya ufasaha lakini itapanda mpaka mahali patakatifu, Yesu anakohudumu. Atayawakilisha kwa Baba bila neno hata moja la kupotosha au la kusitasita, yakiwa yenye harufu nzuri ya ukamilifu wake. Njia ya unyofu na uadilifu huwa haikosi kizuizi, lakini katika kila tatizo yatupasa tuone haja ya wito wa kuwa na maombi. Yesu alisema “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno kwa jina langu,nitalifanya.”TVV 378.1

    Katika jina lake Kristo, wafuasi wake watasimama mbele za Mungu. Kwa sababu ya kuvikwa haki ya Kristo, mwenye dhambi ndani yao. Yeye hutambua sura ya Mwanaye ndani yao ambaye wao humwamini.TVV 378.2

    Bwana husikitika watu wake wanapojihafifisha. Mungu aliwataka la sivyo asingemtuma Mwana wake katika utume ghali wa kuwakomboa. Yeye hupendezwa na watu wanapomtafuta ili kulitukuza jina lake. Wanaweza kutumaini kuona matendo makuu ikiwa watakuwa na imani katika ahadi zake. Lakini kuomba katika jina la Kristo kuna maana kwamba tunapaswa kutenda kazi zake. Mwokozi huokoa watu, siyo katika dhambi bali kutoka dhambini; na wale wanaompenda huonyesha upendo wao kwa utii. Utii wote wa kweli kutoka moyoni. Kwa Kristo ilikuwa ni kazi ya moyoni. Kama tukikubali ataunganisha mioyo yetu na nia zetu pamoja na mapenzi yake tutawezeshwa kiasi kwamba tunapomtii tutakuwa tunatekeleza msukumo ulio ndani yetu. Tutakapomfahamu Mungu kadiri tupatavyo nafasi kumfahamu, maisha yetu yatakuwa mtiririko wa utii. Kwa kushirikiana na Mungu,dhambi zitakuwa chukizo kwetu.TVV 378.3

    Jinsi Kristo alivyoishi hali ya kibinadamu akitii sheria, ndivyo nasi tutaishi kama tukiushikilia Mkono wa nguvu wa imani. Lakini hatuwezi kutegemea mashauri ya wanadamu. Bwana atatuelekeza kutenda wajibu utupasao kama anavyopenda kuwaelekeza wengine pia. Tukimwendea kwa imani atatuzungumzia siri zake binafsi. Wale wanaokataa kutenda kitu cho chote cha kumchukiza Mungu baada ya kumwomba watajua jambo la kufanya. Na watapokea siyo tu hekima, bali pia nguvu uwezo wa kutii, na kufanya kazi watapewa kama Kristo alivyoahidi.TVV 378.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents