Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Udhalimu bila Kiasi

  Katika vizazi vyote, majaribu ya mwili humharibu mtu, hasa kwa kutokuwa na kiasi. Na Shetani hufanya kazi kwa njia ya kuleta udhalimu na kuharibu uwezo wa akili, na kuwafanya watu wawe kama wanyama. Na kwa hiyo watu hupumbaa hata wasiweze kuthamini mambo ya milele. Kwa njia ya uasherati Shetani hutaka kung’olea mbali kila wazo lielekezalo kwa Mungu.TVV 60.2

  Kristo alisema kuwa kabla ya kuja kwake mara ya pili, hali ya ulimwengu itafanana na ile iliyokuwako kabla ya gharika, na ile ya Sodoma na Gomora. Kwetu sisi, fundisho la kufunga kwa Yesu, lazima lizingatiwe kwa makini. Kwa njia ya maumivu yasiyosemekana ya Kristo, ndiyo tutaweza kutambua na kupambanua ubaya wa kutokuwa na kiasi. Tumaini letu tu ni kuteka nyara uchu wa chakula na tamaa na kuvileta chini ya Kristo, na kupatana na mapenzi ya Mungu.TVV 60.3

  Kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kushinda hali ya uasi, ambayo ni asili yake. Lakini kwa njia yakupita katika njia ya Yesu aliyotuandalia tutaweza kushinda. Yesu hatatuacha tuwe wenye hofu na kukata tamaa. Asema, Jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu.” Yohana 16:33.TVV 60.4

  Hebu mtu yule anayeshindana na uchu wa chakula amtazame Mwokozi huko jangwani katika majaribu. Mwangalie huko msalabani katika maumivu makuu huku akilia na kusema, “Nina kiu” Ushindi wake ni wetu pia.TVV 60.5

  Yesu alisema, “Mkuu wa ulimwengu huu anakuja, wala hana kitu kwangu.” Yohana 14:30. Hakuna kitu kilichomhusu Shetani, ambacho Yesu alikuwa nacho. Hakushiriki katika dhambi. Hakukubaliana na dhambi ingawa kwa mawazo tu. Hivyo ndivyo itupasavyo na sisi tuwe. Ubinadamu wa Kristo uliungana na Uungu; aliwezeshwa kushindana kwa Roho Mtakatifu aliyekuwa akikaa ndani yake. Naye alikuja ili kutushirikisha na Uungu. Mkono wa imani wa Mungu unatushika na kutuongoza katika Uungu ulioko kwa Kristo, ili tupate ukamilifu wa tabia.TVV 60.6

  Jinsi jambo hili linavyotimilika, Kristo ametuonyesha. Je, Kristo alimshinda Shetani kwa njia gani? Alimshinda kwa njia ya Neno la Mungu. Alisema, “Imeandikwa.” Kila ahadi iliyomo katika Neno la Mun,gu ni yetu. Soma 2 Petro 1:4. Ukichambuliwa na majaribu, tazama uwezo wa Neno. Uwezo wote wa Neno ni wako. Zaburi 119:11; 17:4.TVV 61.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents