Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wanyama walitunzwa sana

    Wapelelezi hawakuthubutu kumjibu Kristo. Walijua kuwa alikuwa akinena yaliyo ya kweli. Wao badala ya kuvunja mapokeo, walihiari kumwacha mtu ateseke ili kumsaidia mnyama awapo katika shida. Mnyama alitunzwa zaidi ya binadamu. Hiki ni kielelezo cha dini zote za uwongo. Huwa zina asili ya kibinadamu ambayo hujitukuza zaidi ya Mungu, lakini matokeo yake humdhili mtu zaidi ya mnyama. Kila mwalimu wa dini ya uongo na watu wake hudharau mahitaji ya wanadamu, masumbuko yao na haki zao. Injili humwinua binadamu juu zaidi kama mtu aliyenunuliwa kwa thamani kuu, yaani damu ya Kristo, nayo huwafundisha watu kuwajali binadamu na kuwashughulikia katika mahitaji yao na katika dhiki zao. Soma Isaya 13:12.TVV 155.4

    Mafarisayo walikuwa wakimwinda Kristo kwa chuki nyingi, wakati yeye alikuwa akiokoa maisha, na kuwaletea wafu furaha na burudiko. Je, ilikuwa halali kuua siku ya Sabato kama walivyokuwa wakipanga kufanya kuliko Yesu alivyoponya siku ya Sabato?TVV 156.1

    Katika kumponya mtu mwenye mkono uliopooza, Yesu aliilaumu kawaida ya Wayahudi, na kuiacha amri ya Mungu ikisimama kama Mungu alivyoamuru. Kristo alisema: “Ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” Yesu aliitukuza Sabato kwa njia ya kufyagilia mbali mapokeo yote, wakati wale waliokuwa wakilalamika kwa Yesu kuwa anavunja Sabato, wao wenyewe walikuwa wavunja Sabato ya Mungu.TVV 156.2

    Wale wanaosema kuwa Kristo aliiondoa Sabato, hudai kwamba alivunja Sabato na kuwahalalisha wanafunzi wake kuvunja pia. Hivyo hushika njia ya Wayahudi walianguka. Kufanya hivyo kutia tofauti kwa maneno ya Kristo, aliyesema, “Nimezishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.” Yohana 15:10. Mwokozi, wala wafuasi wake hawakuivunja Sabato. Akiangalia watu ambao watamshitaki, alisema: “Nani kwenu anishuhudiaye kwamba nina dhambi?” Yohana 8:46.TVV 156.3

    “Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya Sabato.” Amri kumi za Mungu, ambazo Sabato ni moja yao, Mungu aliwapa watu wake ili wapate mibaraka. Soma Torati 6:24. Wote wanaotunza “Sabato wasiinajisi”, Bwana asema, “Watu hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu. nitawafurahisha katika nyumba yangu ya sala.” Isaya 56:6, 7.TVV 156.4

    “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” maana yote hii ilifanywa naye na pasipo Yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.” Yohana 1:3. Kwa kuwa Kristo alifanya vitu vyote, alifanya na Sabato pia. Kwa ajili yake ilitengwa kando iwe ukumbusho wa uumbaji. Humtaja kuwa ni Mwumbaji na Mtakasaji. Sabato hueleza kuwa aliyeumba vyote ndiye Mkuu wa kanisa, na kwa ajili yake na uwezo wake twapatanishwa na Mungu. Asema: “Niliwapa Sabato zangu kuwa ishara kati yangu na wao, wapate kujua kuwa mimi Bwana Mungu niwatakasaye kuwafanya watakatifu.” Ezekiel 20:12. Sabato ni ishara ya uwezo wa Kristo ututakasao. Nayo ni ishara kwa wote wanaotakaswa na Kristo.TVV 156.5

    Wote wanaopokea Sabato ni ishara ya uwezo wa uumbaji na ukombozi, itapendeza. Isaya 58:13, 14. Angalia Kristo ndani yake. Hupendeza kwake. Inapomkumbusha mpotevu Edeni iliyopotea, amani hiyo itarudishwa kwa njia ya Mwokozi. Kila kiumbe kitakariri mwito: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao, na wenye mzigo mizito, nami nitawapumzisha.” Mathayo 11:28.TVV 157.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents