Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    62 — Mariamu Ampaka Yesu Mafuta

    Simoni wa Bethania alikuwa mmojawapo wa Mafarisayo wachache waliojiunga na wafuasi wa Yesu dhahiri. Alitumaini kuwa Yesu bila shaka ni Masihi, ila hakumwamini kuwa ni Mwokozi. Tabia yake haikubadilika, na kanuni zake zilikuwa zile zile.TVV 311.1

    Simoni alikuwa ameponywa ukoma, naye alitamani kuonyesha shukrani yake. Katika safari ya mwisho ya Kristo ya kutembelea Bethania, Simon alimfanyia makaribisho rasmi pamoja na wanafunzi wake. Makaribisho haya yalihudhuriwa na Wayahudi wengi waliotaka kuona mwenendo, wake, na wengine wasiokuwa rafiki zake.TVV 311.2

    Kama kawaida ya’Mwokozi ilivyokuwa, alikwenda kwa Lazaro kupata mapumziko. Watu wengi walikuja Bethania, wengine kumtaka Yesu, na wengine kumwona Lazaro aliyefufuliwa katika wafu. Lazaro alitangaza kwa uthabiti kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu.TVV 311.3

    Watu walikuwa na shauku kuona ikiwa Lazaro, ataambatana na Yesu mpaka Yerusalemu, na kama nabii atatawazwa kuwa mfalme wakati wa sikukuu ya Pasaka. Makuhani na wakuu wasingekuwa na subira ya kungoja wakati mwingine wa kumwondoa Yesu kutoka katika njia yao. Wakikumbuka jinsi alivyogutusha mipango yao ya mauaji na walikuwa na wasiwasi kuwa labda hatakuja. Waliulizana wenyewe: “Mnafikirije, hawezi kuja: katika sikukuu?”TVV 311.4

    Baraza ikaitwa. Tangu kufufuliwa Lazaro mawazo ya watu wengi yalimuunga mkono Kristo kiasi kwamba lisingekuwajambo la busara kumkamata Yesu waziwazi. Kwa hiyo wakuu waliazimia kumkamata kwa siri, na kumshitaki na kumhukumu kimya kimya. Walitumaini kuwa hukumu yake itakapojulikana msimamo genge wa makutano utawaunga mkono. Lakini kwa kuwa Lazaro anaishi, makuhani na marabi walijua kuwa hawangekuwa salama. Kuwepo kwa mtu aliyekuwa amekufa kwa siku nne, na kufufuliwa kwa neno la Yesu atasababisha upinzani mkubwa kwao. Watu wangelipiza kisasi dhidi ya wakuu wao kwa kumwua Mtu aliyefanya mwujiza wa nanma hiyo. Baraza la Sanhedrini likaamua kuwa hata Lazaro pia lazima auawe.TVV 311.5

    Wakati mpango wa njama hii ulipokuwa ukipangwa huko Yerusalemu, Yesu na wanafunzi wake walikuwa katika makaribisho kwa Simoni. Katika makaribisho haya Simoni aliketi upande mmoja wa Mwokozi, na Lazaro upande wa pili. Martha alihudumu, lakini Mariamu alikuwa akisikiliza maneno ya Mwokozi, maana Yesu alikuwa amemsamehe dhambi zake, na kumfufua kaka yake, kwa hiyo moyo wa Mariamu ulikuwa umejaa shukrani tele. Alikuwa amemsikia Yesu akizungumza juu ya kukaribia kwa kifo chake, naye alitamani kumuonyesha heshima yake.TVV 312.1

    Alikuwa amegharamia kununua kisanduku cha marhamu ambacho ni cha ghali sana, ili kitumike kuupaka mwili wake. Lakini sasa uvumi ulienea kuwa atatawazwa kuwa mfalme. Huzuni ya Mariamu iligeuka kuwa furaha, naye alitaka awe mtu wa kwanza kumheshimia Bwana wake. Alikileta kichupa cha marhamu akikivunja na kummwagia Yesu mafuta kichwani na miguuni, na kisha akapiga magoti huku akilia, na kumlowesha kwa machozi yake, kisha kumfuta kwa nywele zake ndefu. Kushughulika kwake kungeweza kusijulikane na mtu, lakini harufu ya manukato ikajaa chumbani, na kutangaza kitendo chake kwa wote waliokaa humo.TVV 312.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents