Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    64 — Watu wa Kuangamia

    Juhudi ya mwisho ya kuusihi Yerusalemu upate kutubu imekuwa kazi bure. Makuhani na wakuu wamesikia sauti ya unabii, wakati walipouliza kuwa, “Huyu ni nani?” Lakini hawakukubaliana nayo kuwa ni sauti ya unabii, inayowaita watubu. Walijaribu kuwanyamazisha watu kwa hasira. Kwa maofisa Warumi waliokuwa katika maandamano, ambao ni maadui wa Yesu, walimlaumu Yesu kuwa analeta fujo ya maasi. Walidhani kuwa atachukua uongozi wa hekaluni, na kutawala katika Yerusalemi kama mfalme wao.TVV 325.1

    Lakini kwa sauti ya upole, Yesu aliwajibu kwamba hakuja kusimamisha ufalme wa duniani. Karibuni atapanda kwenda kwa Babaye, na adui zake hawatamwona tena, mpaka atakapokuja tena katika utukufu. Hapo basi, wakiwa wamechelewa mno ndipo watakapomkiri.TVV 325.2

    Yesu aliyasema maneno haya kwa masikitiko sana. Wakuu wa Kirumi walinyamazishwa kimya. Mioyo yao iliwaka sana. Katika uso wa Yesu waliona hali ya upendo na Uungwana. Wakaona hali ya huruma katika mioyo yao, kwa jinsi wasivyoweza kuelewa; wakamheshimu sana. Walipowaona makuhani na wakuu, waliwaona kuwa watu wakaidi na wafedhuli sana.TVV 325.3

    Wakati ule ule Yesu alitoweka, akaenda hekaluni. Mahali hapo palikuwa kimya, kwa kuwa maandamano yaliyoelekea katika mlima wa mizeituni, yamevuta watu huko. Yesu alibaki mwenyewe kwa muda kitambo akiliangalia hekalu kwa masikitiko. Kisha alirudi kwenda Bethania. Watu walipomtafuta wamtawaze, hakuonekana.TVV 325.4

    Usiku kucha Yesu alikuwa akiomba. Kulipopa-mbazuka alirudi hekaluni tena. Alipokuwa njiani, aliona njaa, “naye aliuona mtini kwa mbali kidogo, umestawi sana. Akaujia akitazamia kupata matunda kwake. Alipoufikia hakupata cho chote kwake, maana wakati wa kuzaa tini haujafika”.TVV 325.5

    Katika nyanda za juu kuelekea Yerusalemu, ni kweli kuwa wakati wa kuzaa tini haujafika, lakini katika viunga ambako Yesu alitokea, mtini mmoja ulionekana kana kwamba umetangulia mingine. Ulikuwa umetanda majani tayari kuweka maua na matunda. Lakini mwoonekano wake ulikuwa udanganyifu tu. Yesu hakuona kitu cho chote juu yake ila majani tu.TVV 326.1

    Kristo aliulaani kwa kusema, “Mtu ye yote asile matunda kwako.” Asubuhi yake Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakirudi njiani, waliona kuwa matawi na majani yake yamenyauka. Petro alisema: “Bwana, tazama mtini ulioulaani umenyauka.”TVV 326.2

    Kitendo cha Kristo kuhusu kulaani mtini kilionekana kwa wanafunzi wake kuwa si kawaida. Walikumbuka maneno yake yasemayo “Mwana wa Adamu hakuja kuangamiza watu, bali kuokoa.” Luka 9:56. Kazi zake hazikuwa za kuharibu, ila za kutengeneza. Kitendo hiki ni cha pekee. Makusudi yake yalikuwa nini? Wanafunzi waliuliza.TVV 326.3

    “Kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, sikufurahii kufa kwake mwovu ...” Ezekieli 33:11. Kwake, maneno ya kutukana, na kulaani ni kazi ngeni, au nl “tendo la kigeni.” Isaya 28:21. Lakini kwa rehema na upendo huinua pazia linalofunika mambo mbele, ili laana ya dhambi ionekane.TVV 326.4

    Mtini uliokauka, uliojionyesha wazi mbele ya Kristo, ulikuwa mfano wa Wayahudi. Kristo alitaka kudhihirisha ajali ya Wayahudi kwa mfano huo wa mtini.TVV 326.5

    Wayahudi walijidai kuwa na haki kuliko mataifa yote. Lakini walikuwa wafedhuli sana na wenye kupenda mapato. Walitangaza madai yao ya udhalimu na kujionyesha kuwa taifa la Kiyahudi ni la haki hasa, lakini halikuwa na lo lote, ila majani tu. Dini ya Wayahudi na hekalu lao mashuhuri pamoja na mipango mizuri ya ibada zao, kwa kweli ilikuwa safi kwa nje tu, lakini unyenyekevu, upendo, na uongofu haukuwako.TVV 326.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents