Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    30 — Awekea Mikono Mitume Kumi na Wawili

    “Ndipo alipanda mlimani, akawaita wale aliowataka, nao wakamjia. Naye akaweka kumi na wawili wawe pamoja naye, ili awatume waende kuhubiri.”TVV 158.1

    Chini ya vivuli vya miti ya milimani, mbali kidogo na pwani ya ziwa la Galilaya, watu kumi na wawili waliitwa ili wapate kuwa mitume, na hapo ndipo tangazo la mlimani lilipotolewa. Katika kuwafunza wanafunzi wake Yesu aliamua kutoka katika ghasia na fujo ya mjini, akaenda mahali pa kimya, katika milima penye utulivu, ili apate kuwafundisha. na katika kazi yake yote, alikuwa akiwakusanya watu mahali pa wazi, katika majani kando ya milima, au kando ya ziwa mahali penye utulivu. Mahali kama hapo ndipo alikuwa akiwaongoza wasikilizaji kwenye viumbe vya asili, hapa angewageuza watu kwa yale mambo yaliyofanywa kwa mikono ya watu kwa yale ya asili. Watu waliweza kujifunza kukua na kuendelea kwa viumbe, na hapo walipata mafundisho ya hakika ya ukweli wa Mwenyezi.TVV 158.2

    Sasa hatua ya kwanza ilikuwa ikichukuliwa kupanga kanisa ambalo baada ya kuondoka kwa Kristo, litakuwa likimwakilisha katika ulimwengu. Hakuna mambo yenye gharama kubwa yaliyohitajika. Bali uzuri na utakatifu wa hali, ambayo watakuwa nayo milele wakiangalia uzuri wa uumbaji katika milima, mabonde, na bahari.TVV 158.3

    Yesu aliwaita wanafunzi wake ili awazoeze na kuwafunza ili baadaye awatume ulimwenguni kutangaza mambo yale waliyoyaona na kusikia kwake. Madaraka waliyopewa yalikuwa muhimu sana ambayo watu hawajapewa kama hayo. Madaraka yao yalikuwa ya pili kwa yale ya Kristo mwenyewe. Kazi yao ilikuwa kushirikiana na Mungu ili kuuokoa ulimwengu.TVV 158.4

    Kristo alijua tabia za watu ambao amewawekea mikono wawe mitume wake; udhaifu wao na makasoro yao yalikuwa wazi machoni mwake. Alijua hatari zilakazowakabili, kwa hiyo aliwahurumia sana. Kila mara aliwaombea wakiwa peke yao juu mlimani usiku kucha; wakati wao walikuwa wamelala chini ya mlima. Asubuhi mapema alikuwa amewaendea tayari.TVV 158.5

    Yohana na Yakobo na Petro, pamoja na Filipo, Nathanael na Mathayo, walikuwa washiriki wa Kristo wa karibu sana, wakiwa watenda kazi wenye juhudi. Petro na Yakobo na Yohana walikuwa washiriki wa karibu zaidi kwa Kristo, wakiona miujiza yake na kusikia maneno yake. Mwokozi aliwapenda wote, lakini Yohana alikuwa mpendwa hasa. Alikuwa kijana zaidi na alikuwa na matumaini ya ujana zaidi. Alifungua moyo wake kwa Yesu kabisa. Hivyo alifadhiliwa sana na Yesu na kupokea mafundisho ya Mwokozi.TVV 159.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents