Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    20 — “Msipoona Ishara na Maajabu”

    Wagalilaya waliorudi kutoka Yerusalemu kwa pasaka, walileta habari za mambo ya ajabu waliyoona kwa Yesu. Watu wengi walilalamika kwa ajili ya kuchafua hekalu, na kwa ajli ya uchoyo na ufidhuli wa makuhani. Walitumaini kuwa mtu huyu aliyewafukuza wakuu hekaluni anaweza kuwa ndiye Mkombozi wao, waliyemtazamia kwa muda mrefu. IIisemekana kuwa nabii Yohana Mbatizaji amejitangaza kuwa ndiye Masihi. Habari za kurudi kwa Kristo kutoka Kana pia, zilienea pote, katika Galilaya. Katika Kapernaumu habari hizi zilimvutia Myahudi mmoja aliyekuwa katika utumishi wa utawala. Mwana wa mtu huyu alikuwa na ugonjwa unaosemekana kuwa hauponyeki. Baba yake aliposikia habari za Yesu, alikusudia kutafuta msaada kwake. Alitumaini kuwa, akimsihi atamhurumia.TVV 104.1

    Alipofika huko Kana, baba huyu alipenyapenya katika mkutano mpaka akamfikia Mwokozi. Imani yake iliweweseka, kwanza alipomwona Yesu akiwa mtu wa kawaida tu, mwenye mavazi ya kawaida, hali amechoka kwa ajili ya safari. Basi alimzungumzia, akamweleza jambo lililomleta kwake. Akamwomba Mwokozi afuatane naye kwenda kwake.TVV 104.2

    Yesu alijua kwamba, moyoni mwake alikuwa akimtakia mwanawe uzima, maana alikuwa akimwamini. Na kama haja yake ikikataliwa hawezi kumwamini kuwa ndiye Masihi. Wakati mtu yule alipokuwa akingoja kwa uchungu, Yesu alisema, “Msipoona dalili na maajabu, hamwezi kuamini.”TVV 104.3

    Mwokozi alitofautisha swali la mwombaji na mashaka na imani kamili ya mwananike wa Samaria ambaye hakuomba ishara wala mwujiza. Maneno yake yalikuwa na uwezo uliowagusa mioyo. Alisikitika kwamba watu wake hasa walishindwa kutambua sauti ya Mungu ikisema ndani ya Mwanawe.TVV 104.4

    Hata hivyo diwani huyo alikuwa na imani kiasi fulani, maana alikuja kuomba msaada, ambao ni jambo muhimu kwake. Yesu alikusudia, si kumponya kijana wake peke yake, ila kuwaongoa watu wote wa nyumba hiyo, na kuwasha mwanga katika Kapernaumu nzima. Lakini diwani huyu lazima atambue haja yake kuu, kabla ya kupata neema ya Kristo. Watu wengi katika taifa lake walimpenda Kristo kwa nia ya ubinafsi. Imani yao kwake ilikuwa kwa ajili ya kupata misaada ya muda tu, lakini hawakuona haja ya neema ya Mungu.TVV 105.1

    Kama kimuli cha nuru, maneno ya Kristo yaliufunua moyo wake ukawa wazi. Akaona kuwa nia yake ilikuwa ya ubinafsi. Haja yake ikafunuliwa kuwa ilikuwa imejifunika katika ganda, kumbe sivyo ilivyo. Akatambua kwa masikitiko kuwa kusitasita kwake kungeweza kugharimu maisha ya mwanawe. Akalia kwa uchungu: “Bwana, shuka nyumbani kwangu, mtoto wangu yumo kufani.” Imani yake ikamshikilia Kristo kama Yakobo alipokuwa akishindana na malaika, alisema: “Sikuachi, usiponibariki.” Mwanzo 32:26 Alishinda sawa na Yakobo. Yesu akasema, Enenda zako, mtoto wako amepona.” Diwani akatoka kwa Yesu akifurahi sana, huku akiwa na amani kamili.TVV 105.2

    Wakati ule ule watu waliokuwa wakimwuguza mtoto waliona mabadiliko ya ghafla kwake. Hali ya homa ikageuka kuwa uzima wa afya safi. Nguvu za mwili zikatokea badala ya udhaifu katika mwili wake. Hakuna dalili yoyote ya ugonjwa iliyosalia kwake. Akapona kabisa, mwili wake ukawa safi, na akaendelea kulala tu. Jamaa yake wakashangaa, ikawa furaha kubwa.TVV 105.3

    Yule diwani angalifika nyumbani wakati wa jioni ile, baada ya kuongea na Yesu, lakini hakuwa na haraka ya kuja nyumbani, mpaka kesho yake ndipo akafika Kapernaumu. Ilikuwa hamu kubwa kiasi gani kwa wote wa nyumbani.TVV 105.4

    Alipomwendea Yesu alikuwa na huzuni kubwa. Sasa hali yake ni tofauti kiasi gani! Aliposafiri katika utulivu wa asubuhi, hali ya nchi ilionekana kuwa inamsifu Mungu, yeye akiwa mmoja wao. Alipokuwa angali kitambo kufika kwake, watumishi walimlaki ili kumtuliza, maana walijua kuwa hali yake ni ya wasiwasi. Hakushtuka kusikia habari walizomletea, ila aliwauliza tu, muda ambao homa ilmwacha. Wakamjibu: “Jana, muda wa saa saba, ndipo homa ilimwacha.” Wakati ule ule imani ya mzee ilipoimarika kwa Yesu; na Yesu akasema: “Mwanao yu hai,” ndipo upendo wa Mungu ulipomgusa kijana aliyekuwa katika kufa.TVV 105.5

    Baba akaharakisha kwenda kumpa pole mwanawe. Alimkumbatia, kama mtu atokaye Kifoni, akamshukuru Mungu tena na tena kwa ajili ya kuponywa kwa ajabu.TVV 106.1

    Baadaye diwani alipozidi kujifunza neno la Mungu, ndipo mji wake wote wakawa wafuasi wa Kristo. Habari za mwujiza huu zikaenea pote, na mji wa Kapernaumu ukatayarishwa kwa kazi ya Kristo.TVV 106.2

    Sisi nasi sawa na baba yule, mara kwa mara humtafuta Yesu ili atusaidie katika mambo ya duniani, na kwa kutupatia haja zetu, humtegemea. Mwokozi anatamani kutupatia mibaraka zaidi kuliko ile tuombayo, naye hukawia kutujibu, ili apate kujua dhambi zetu, na kuona haja zetu kubwa za neema yake. Anataka tuondoe ubinafsi unaotufanya tumwendee.TVV 106.3

    Diwani alitaka kuona utimilifu wa haja yake kwanza kabla hajamwamini lakini inampasa aliamini neno la Mungu kwamba maombi yake yamesikiwa, na haja yake itatolewa. Siyo kujisikia au kuona kuwa Mungu atusikia ndipo tuamini. Yatupasa kuziamini ahadi zake. Tunapomwomba, lazima tuamini kuwa tunapokea tuliyoomba, na tushukuru ya kuwa tumepokea. Kisha tuendelee katika shughuli zetu tukijua kuwa haja zetu zitatujia wakati tuzihitajipo zaidi.TVV 106.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents