Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kina na Upana wa Sheria ya Mungu

    Yesu alizichukua amri moja moja na kuelezea kanuni zake jinsi zilivyo. Alisema kwamba mawazo mabaya, au mtazamo wa kutamani ni kuvunja amri ya Mungu. Kutenda jambo dogo tu ambalo si la haki ni kuvunja sheria. Mtu anayeruhusu chuki katika moyo wake, huwa ameweka miguu yake katika njia ya kuua.TVV 167.1

    Wayahudi walitunza roho za kulipa kisasi, yaani ovu kwa ovu. Katika hali yao ya kuwachukia Warumi, walikuwa wakitoa matusi ovyo ovyo, hali wamejizoeza kutenda amtendo maovu. Kuna mambo ya kutia uchungu ambayo huhalalishwa hata kwa wafuasi wa Kristo. Wanapoona kuwa jina la Mungu linadharauliwa, au wenye haki wakitendewa ukatili, hasira yao huchochewa. Hasira kama hizo si dhambi. Lakini uchungu na hasira za kawaida, lazima ziondolewe katika watu wanaoelekea mbinguni.TVV 167.2

    Mawazo ya Mungu kwa watoto wake ni ya juu mno kuliko mawazo ya kibinadamu yaliyo bora mno. “Mwe wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. Amri hii ni ahadi. Mpango wa ukombozi hutaka kuondolewa kabisa mikononi mwa Shetani. Kila mara Kristo humtenga kabisa mtu yule anayetubia dhambi zake. Amepanga kwamba Roho Mtakatifu atamjia kila mtu anayetubu, na kumtunza asifanye dhambi tena.TVV 167.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents