Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wasamaria waliamini upendo wa Yesu

  Katika agizo la Yesu kwa wanafunzi wake kabla ya kupaa kwenda mbinguni, alitaja Samaria pamoja na Yerusalemu na Uyahudi mahali alipokuwa akifanyia kazi, ya kuhubiri Injili. Walipofika Samaria walikuta watu wako tayari kuamini. Wasamaria waliona kwamba ijapokuwa hawakumtendea Yesu vizuri, lakini alikuwa akiwafikiria mambo ya heri, kwa hiyo waliamini neno la Mungu. Baada ya kupaa kwake kwenda mbinguni, wanafunzi wake walipata mavuno makubwa ya waongofu kwa watu waliokuwa na uhasama kwao. “Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima, hukumu duniani.” Isaya 42:3.TVV 277.2

  Katika kuwatuma watu sabini, Yesu aliwaagiza kuwa wasiwalazimishe watu ili wawakaribishe. “Katika mji wowote mwingiamo, wasipowakaribisha tokeni humo na kukung’uta mavumbi ya miguu yenu, na kusema kuwa mavumbi haya yatawashuhudia mbele za Mungu” Haikuwapasa kufanya hivyo kwa hasira, ila kwa masikitiko ya kuwakataa wajumbe wa Bwana. Kuwakataa wajumbe wa Bwana ni sawa na kumkataa Kristo mwenyewe.TVV 277.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents