Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    67 — Yesu Azuru Hekalu Mara ya Mwisho

    Ilikuwa siku ya mwisho ya Yesu kufundisha hekaluni. Kijana wa Kigalilaya alisimama, akiwa hali ya kawaida tu. Akizungukwa na makuhani wenye hali ya kitajiri sana, na wakuu wenye mavazi ya fahari sana na mapambo ya kila hali, na Waandishi wakishikilia mkononi mwao magombo waliyoyafunua kila mara. Yesu alisimama kimya kama mwenye kuvikwa uwezo wa kimbingu. Aliwakodolea macho adui zake, waliokuwa na uchu wa uhai wake. Mitego yao ya kutaka kumnasa ikiwa imeshindwa. Alikuwa amekutana na maswali mbali mbali, akitoa majibu safi ya hakika, kinyume cha giza la makosa ya Mafarisayo na Makuhani. Maonyo yalitolewa kwa uaminifu. Walakini ilibakia kazi nyingine kwa Kristo, kufanya.TVV 342.1

    Watu walikuwa wamefurahishwa na mafundisho yake, ingawa walikuwa na wasiwasi. Walikuwa wakiwatumaini Makuhani na Waalimu, lakini sasa wanawaona watu hawa wakimwinda Yesu, kumdhalilisha ambaye maarifa yake yalitoa nuru ya kila shambulio. Walishangaa kwa kuwa Makuhani na Marabi hawakumwamini Yesu, ambaye mafundisho yake yalikuwa dhahiri na rahisi kueleweka. Wao wenyewe hawakujua njia ya wima ya kufuata.TVV 342.2

    Katika mifano, lilikuwa kusudi la Kristo kuwaonya wakuu na kuwafundisha watu ukweli. Lakini ilikuwa ni lazima kusema kwa wazi zaidi. Kutokana na imani yao duni kwa ukuhani, uliopotoshwa, watu walikuwa wametekwa. Kristo lazima akate minyororo hii. Alisema: “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, basi yo yote watakayowaambieni myashike na kuyatenda, lakini msiwaige jinsi wanavyokuwa, maana kwao hunena tu, wala hawatendi hivyo wanavyonena.”TVV 342.3

    Waandishi na Mafarisayo waliamua kukichukua kiti cha Musa, wakiwa kama ndio wenye kufundisha sheria, lakini hawakufanya kama sheria isemavyo. Na walifundisha mengi yaliyo kinyume cha Maandiko Matakatifu. Wao hufunga Mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitende wenyewe kugusa kwa kidole chao. Hufundisha sheria, na kuwalazimisha watu wazishike, wao hujidai kusamehewa wasitenda hivyo.TVV 342.4

    “Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu Rabi. Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoia, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.”TVV 343.1

    Katika maneno ya wazi kama hayo Mwokozi alidhihirisha tamaa ya ubinafsi iliyokuwa inajikweza kutaka makuu kila mahala, huku ikionyesha kejeli ya unyofu, na huku moyo umejaa wivu na choyo. Mafarisayo walikuwa wakitafuta kwa kila hali kujionyesha na kujipendelea. Mambo kama hayo yalikemewa na Yesu.TVV 343.2

    Alikemea ubatili uliyoonyeshwa katika kutamani kuitwa Rabi, au Bwana. Makuhani, Waandishi na Wazee, wote walikuwa ni ndugu, watoto wa Baba mmoja. Watu hawakupaswa kumpa mtu ye yote heshima ya kuwafanya watawaliwe nia zao, au imani yao.TVV 343.3

    Kama Kristo angelikuwako ulimwenguni leo, akizungukwa na watu wenye majina ya heshima kama vile Mstahiki (Reverend), au Mstahiki Sana (Right Reverend), je, asingaliurudia usemi wake kwamba Msiitwe bwana, kwa kuwa mnaye Bwana mmoja ndiye Kristo?” Maandiko Matakatifu humtaja Mungu kuwa, jina lake ni Takatifu na la kuogopwa.” (Zaburi 119:9). Watu wangapi hujiita kwa jina hilo linalomhusu Mungu na huku wakiwakilisha vibaya jina na tabia yake. Mara ngapi tamaa za kidunia na dhambi mbaya kabisa zimefichwa ndani ya vazi la cheo cha juu na kitakatifu!TVV 343.4

    Mwokozi aliendelea kusema: “Atakaye kuwa mkubwa wenu, atakuwa mtumishi wenu. Atakaye-jikuza atashushwa, na atakayejidhili atakuzwa.” Kristo alifundisha mara nyingi kwamba, ukuu wa kweli hupimwa katika hali ya unyofu. Mbele ya mbingu ukuu halisi hupimwa kwa jinsi mtu anavyowahudumia wanadamu wenzake. Kristo ambaye ni Mfalme wa utukufu alikuwa mtumishi wa wanadamu wenye dhambi.TVV 343.5

    “Mnawafungia watu wasiingie katika ufalme wa mbinguni, ninyi wenyewe hamwingii, na wanaotaka kuingia mnawazuia.” Kwa njia ya kuyapotosha Maandiko Matakatifu makuhani na wanasheria waliwazuia watu wasielewe njia ya kuingia katika ufalme wa mbinguni.TVV 343.6

    “Mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnaomba sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa zaidi.” Mafarisayo walipata heshima ya wajane watauwa, na walifanya kuwa ni kawaida yao kuchukua vitu vyao kwa ajili ya makusudi ya dini. Baada ya kupata fedha zao walizitumia kwa faida yao. Ili kujificha na upotovu wao waliomba sala ndefu sana na kujionyesha kuwa ni watu wa dini kamili. Makaripio ya aina hiyo yanawahusu watu wa sasa pia. Maisha yao yamejaa ubinafsi na uovu, walakini hujifunika na vazi la dini, waonekane kana kwamba ni wenye dini halisi.TVV 344.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents