Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  41 — Hatari Katika Galilaya

  Kristo alijua ya kuwa wakati wa kazi yake ulimwenguni ulikuwa ukingoni kumalizika, makundi ya watu wanamtukuza leo na kumtaka awe mfalme, kesho watamgeuka. Hoihoi za kibinafsi zinazoonekana leo, kesho zitageuka kuwa chuki isiyotaka kuona kazi hiyo.TVV 211.1

  Walakini hakuchukua hatua yoyote ya kuepukana na hatari hiyo. Tangu mwanzo hakuwa na tumaini lolote la kupata thawabu duniani, katika wale wanaoungana naye sasa, walikuwa wamevutiwa na utukufu wa duniani, yaani kutumaini kupata chochote katika ufalme wa duniani. Hawa lazima wamefahamu kuwa Yesu hana nia ya ufalme.TVV 211.2

  Kesho yake asubuhi na mapema watu walikusanyika wengi sana huko Bethsaida. Wale waliomwacha yesu ng’ambo kule, walienda huko tena wakitumaini kumkuta huko, maana haikuwapo mashua yoyote ambayo ingalimchukua. Lakini tumaini lao lilikuwa bure.TVV 211.3

  Wakati huo alikuwa amefika, Genesareti baada ya kutokuwapo siku moja. Wale waliotoka Bethsaida walipata habari kwa wanafunzi wake kuwa alivuka bahari kwa miguu. Walieleza jinsi tufani ilivyokuwa kubwa, jinsi walivyosumbuka kwa masaa mengi ndani ya upepo mkali, na jinsi Kristo alivyokuwa akitembea majini, na jinsi Yesu alivyotuliza tufani kwa neno lake, watu walitaka maelezo zaidi juu ya miujiza hiyo kutoka katika kinywa cha Yesu mwenyewe.TVV 211.4

  Yesu hakuwaambia maneno ili kuwaridhisha. Alisema tu kwa masikitiko: “Mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, ila kwa kuwa mlikula mikate mkashiba. Msikitendee kazi chakula kiharibikacho, ila kile kidumucho hata uzima wa milele.” Msitafute faida isiyodumu, bali tafuteni chakula cha kiroho kidumucho.TVV 211.5

  Usikizi wa watu uliamshwa kwa muda kitambo, kwa hiyo wakauliza wakisema: “Tutafanyaje ili tutende kazi za Mungu?” Maswali yao yalihusu kwamba: Tufanyeje ili tufike mbinguni? Tutahitajika kulipa gharama gani ili tupate uzima ujao?TVV 211.6

  Kwa maswali haya yesu alijibu akisema: “hii ndiyo kazi ya Mungu, Mwaminini yule aliyetumwa naye.” Gharama ya kufika mbinguni ni Yesu. Njia ya kufika mbinguni ni kuwa na imani, au ni kumwamini Mwana Kondoo wa Mungu.TVV 212.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents