Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    13 — Ushindi

    “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, kisha akamwambia: “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini, maana imeandikwa: Atakuagizia malaika zake wakulinde, na mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.”TVV 62.1

    Shetani alikuwa bado anaonekana kama malaika wa nuru. Alijionyesha kuwa anajua maandiko. Jinsi Yesu alivyotumia maandiko kumsaidia, ndiyo mjaribu huyu alivyoyatumia pia kukamilisha ukamilifu wake. Shetani alimdai Mwokozi aonyeshe ushahidi zaidi kwamba ni Mwana wa Mungu.TVV 62.2

    Lakini tena jaribu hili liliambatana na mashaka ya kutoamini: “Kama wewe ni Mwana wa Mungu.” Kristo, alijaribiwa, “Kama”, lakini yeye aliepuka kuonyesha mashaka ya kutoamini.TVV 62.3

    Shetani alitaka kumtegatega na kumshinda, kwa kuwa ni mwanadamu. Akamtaka ajionyeshe, yaani ajivune. Lakini ajapokuwa Shetani hushawishi ili tu atende dhambi, hawezi kumlazimisha mtu. Alisema, “Jitupe chini”, hali akijua kuwa hawezi kumtupa chini, wala kumlazimisha ajitupe chini. Kristo asipokubaliana na jaribu hilo, hawezi kulitimiza, ila atashinda.TVV 62.4

    Mjaribu hawezi kamwe kutulazimisha tutende dhambi. Dhamiri lazima ikubali, imani lazima ianguke kwa Kristo, ndipo Shetani hurumia hila zake juu yetu. Lakini kila aina ya tamaa tunayopendelea, ndiyo mlango tunaofungua ili mjaribu atuingilie kutuharibu. Na kila kushindwa kwetu tunakoshindwa, humdhihaki Kristo. Wakati Shetani alipotumia neno lile kwamba, Atakuagizia malaika, aliacha maneno yasemayo, “akulinde katika mapito yako yote”. Maana yake, wakulinde katika mapito yale yaliyoamriwa na Mungu. Yesu alikataa kwenda kinyume na maagizo ya Mungu. Kama angeruka, asingalitazamia hifadhi kumjia. Na hivyo asingalikuwa kiele kwa wanadamu.TVV 62.5

    Yesu alimwambia Shetani, “Imeandikwa tena Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Mungu alikuwa ametangaza wazi kuwa yeye ni Mwanawe. Sasa kutaka kithibitisho ni kulijaribu Neno la Mungu, yaani kumjaribu Mungu. Tusitoe maombi yetu kwa Mungu kwa kujaribu kuona kuwa atafanya au namna gani. Atafanya kama alivyosema kwa sababu anatupenda. Soma Waebrania 11:6. Majivuno ni maigizo ya Shetani kwamba ndiyo imani. Imani ni ile inayodai ahadi za Mungu, na huleta matunda ya utiifu. Majivuno pia hudai ahadi za Mungu, lakini huzitumia katika kuasi. Imani ingewaongoza wazazi wetu wa kwanza kuutegemea upendo wa Mungu, na kutii sheria zake; wakiamini kuwa pendo lake kuu litawaokoa kutoka dhambini. Hakuna imani inayodai fadhili za Mungu, bila kuambatana na masharti ambayo rehema za Mungu hutolewa.TVV 63.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents