Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Pilato Hakuweza Kuona Matokeo ya Baadaye

    Pilato hakudhani kuwa itakuwa hivyo. Alinywea kwa hofu kumtoa mtu asiyekuwa na hatia akateswe na kuuawa kifo cha ukatili kuliko vyote. “Kwani ni ubaya gani alioutenda? Lakini shauri lilikuwa limekwenda mbali kikomo cha ubishi Hata hivyo Pilato alijitahidi kumwokoa Kristo. “Akawaambia mara ya tatu, kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani?” Lakini kule tu kutaja kufunguliwa kwake, kuliwatia watu wazimu. wakazidi kupaza sauti, “asulubiwe, asulubiwe!”TVV 415.1

    Yesu akiwa mwenye kuzimia na majeraha, alipigwa mijeledi. “Nao askari wakamchukua ndani ya behewa, ndiyo Praitorio; wakamkusanya kikosi kizima. Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani mwake; wakaanza Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” Wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudia.” Mara kwa mara mkono wa mkorofi mmoja ulimpiga kichwani na kukandamiza taji ya miiba katika paji lake, na kufanya damu itiririke usoni.TVV 415.2

    Kundi hilo lililokuwa kama lenye wazimu lilimsonga Mwokozi wa ulimwengu. Dhihaka na kejeli vilichanganyikana na makufuru. Shetani aliongoza kundi hili. Lilikuwa kusudi lake kumchokoza Mwokozi mpaka arudishe kwa ukali kama ikiwezekana, au kumlazimisha atende muujiza na kujiokoa. Doa moja katika maisha yake kama mwanadamu na Mwana Kondoo wa Mungu angekuwa kafara yenye kasoro na hivyo wokovu wa mwanadamu utakuwa umeshindikana. Lakini alijitoa na kwa uvumilivu akastahimili dhihaka na uovu wote.TVV 415.3

    Maadui za Kristo walikuwa wamedai ishara kama uthibitisho wa Uungu wake. Walikuwa na ushahidi tosha kabisa kuliko waliomtafuta. Unyofu na uvumilivu wake vilithibitisha udugu wake na Mungu. Matone ya damu yaliyokuwa yanadondoka kutoka katika majeraha usoni pake yalikuwa ni amana ya kupakwa “Mafuta ya shangwe” kama Kuhani wetu Mkuu. (Soma Waebrania 1:9). Hasira ya Shetani ilikuwa kali wakati alipoona kuwa katika kila jambo Mwokozi ametimiza mapenzi ya Baba yake.TVV 415.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents