Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Alitendewa kama tulivyostahili

  Kristo alitendewa jinsi tulivyostahili sisi, ili sisi tutendewe kama alivyostahili Yeye. Alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu, akashiriki adhabu yetu ili sisi tuhesabiwe haki yake, ambayo sisi hatuna ushirika nayo. Alikufa kifo chetu, ili sisi tupate uzima wake. “Kwa kupigwa kwake tumepona.” Isaya 53:5.TVV 12.4

  Lilikuwa kusudi la Shetani kuleta utengano wa milele baina ya Mungu na watu, lakini kwa kutwaa hali ya kibinadamu, Kristo Mwokozi wetu alijiungamanisha na watu kwa kifungo kisichoweza kukatika kamwe.’ Mungu aliupend aulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee’ Yohana 3:16. Alimtoa si kwa kutufia tu, bali kwa kujiungamanisha na ubinadamu milele.TVV 13.1

  “Kwa ajili yetu amezaliwa mtoto, ukuu utakuwa begani mwake.” Mungu amejitwalia ubinadamu kwa njia ya Mwanawake, naye amechukua hali hiyo mpaka katika mbingu za juu kabisa. “Mwana wa binadamu” ataitwa wa ajabu, Mshauri wa ajabu, Mungu hodari, Baba wa milele, Mkuu wa amani.’ Isaya 9:6. Yeye aliye mtakatifu, asiyekuwa na doa lolote, asiyechafu-liwa na kitu chochote, ajitengaye na dhambi, haoni haya kutuita sisi ndugu zake. Waebrania 7:26; 2:11. Mbinguni kunahusiana na ubinadamu, na ubinadamu unakumbatiwa na mbingu kwa upendo.TVV 13.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents