Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi kila mtu atakavyo jihukumu

    Pale katika msalaba wa Kalwari, upendo na ubinafsi ulisimama uso kwa uso. Yesu aliishi tu kuwabariki na kuwafariji, na kule kumwua, Shetani alidhihirisha chuki yake kwa Mungu. Asili ya uasi wake ni kumwondoa Mungu, na kumharibu Mwana wa Mungu.TVV 26.6

    Kwa maisha ya kifo cha Kristo, mawazo ya wanadamu yalipambanuliwa. Maisha ya Yesu yalikuwa ni wito wa kujitoa nafsi na kushirikiana katika taabu. Wote waliomsikia kwa Roho Mtakatifu walivutwa kwake. Wanaoabudu nafsi na wa utawala wa Shetani. Katika mtazamo wao kwa Kristo, watajidhihirisha wanakosimama. Kwa njia hii kila mtu atajihukumu mwenyewe.TVV 27.1

    Siku ya mwisho ya hukumu, msalaba utasimamishwa, na kuhusika kwake kwa watu kutaonekana kwa kila mtu. Kabla njozi ya msalaba wa Kalwari na yule aliyesulubishwa kwake, wenye dhambi watasimama, huku wamehukumiwa tayari. Watu wataona matokeo ya uchaguzi wao. Kila swali kuhusu mashindano haya litakuwa dhahiri. Mungu hataonekana na lawama yoyote kuhusu maendeleo ya dhambi, na asili ya dhambi. Itaeleweka kwamba katika serikali ya Mungu, hakuna kasoro yoyote, wala hakuna sababu ya kunung’unika. Wote wenye haki na waasi pia watasema: “Ni za haki, na za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu . . . Hukumu zao zimedhihirika.” Ufunuo 15:3, 4.TVV 27.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents