Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    58 — Kufufuliwa kwa Lazaro

    Miongoni mwa wanafunzi wa Yesu wa maana sana, mmojawapo alikuwa Lazaro wa Bethania, naye alikuwa mpendwa mkubwa wa Mwokozi. Kwa Lazaro ndiko mwujiza mkubwa wa Yesu ulifanyika. Mwokozi aliwapenda wanadamu wote, lakini kwa wengine aliwashiriki zaidi.TVV 295.1

    Nyumbani kwa Lazaro ndiko Yesu alilala mara nyingi. Mwokozi hakuwa na nyumba yake. Alipochoka, au kuwa na kiu au njaa, kama binadamu wote, kila mara alikwenda katika mji huo, ambapo alikaribishwa na kupafanya kana kwamba ni kwao.TVV 295.2

    Makutano walipomfuata Kristo mahali pa wazi aliwaeleza kuhusu uzuri wa viumbe hasa miti na mimea. Lakini makutano hawakuwa wepesi wa kuzingatia. Na katika Bethania, Yesu alipata mahali pa kupumzikia, baada ya shughuli za mchana. Hapa hapakuwa na haja ya kusema kwa njia ya mifano.TVV 295.3

    Kristo alipokuwa akitoa mafundisho yake ya ajabu, Mariamu alikuwa akipenda miguuni pake na kumsikiliza. Wakati fulani Kristo alipokwenda Bethania kama mgeni, mara ya kwanza, Martha aliyekuwa akipika, alimwendea Yesu, na kumwambia kuwa amwambie Mariamu ili amsaidie. Yesu alijibu, akasema: “Martha, Martha, unajisumbua na mambo mengi: Lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu alichagua fungu lililo jema, ambalo halitaondolewa.’ Martha asingalihangaika sana kwa mambo yanayo-pita, ila ahangaikie mambo ya milele. Martha anahitaji maneno ya Kristo, kama Mariamu, kabla ya kushughulika na mambo mengine. Kwanza apate mibaraka ya Kristo.TVV 295.4

    Huzuni ilianguka katika mji ambao ulikuwa mapumziko ya Yesu. Lazaro alishikwa na ugonjwa wa ghafla, na dada zake walituma habari kwa Yesu wakisema: “Bwana tazama yule umpendaye hawezi sana.” Waliona ugonjwa uliomshika ndugu yao ulikuwa mkubwa sana, lakini walijua kuwa Yesu amejionyesha kuwa na uwezo wakuponya magonjwa ya kila namna. Hawakumwita kwa haraka sana, ila walitaka aende Bethania kwa upesi inavyowezekana.TVV 295.5

    Walingoja kwa subira kubwa kwa kadiri ya ugonjwa ulivyozidi kuwa mkubwa kwa ndugu yao. Walimwombea sana na kumsubiri Mwokozi. Lakini mtu aliyetumwa kwake alirudi mwenyewe, bila Kristo, lakini, alituma ujumbe akisema: “Ugonjwa huu sio wa mauti”, kwa hiyo walitumaini kuwa Lazaro atapona. Mgonjwa alipofariki walisikitika vikubwa sana, lakini” walijisikia kuwa na tumaini katika Kristo.TVV 296.1

    Yesu aliposikia habari hizo hakuonyesha huzuni, kama vile wanafunzi wake walivyotazamia kuona. Alisema tu kwamba: ‘Ugonjwa huu sio wa mauti, ila ni wa kumtukuza Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe.” Yesu alikawia muda wa siku mbili. Kukawia huku kulikuwa fumbo kwa wanafunzi wake, kwa kuwa waliwapenda watu wa jamaa hiyo ya Bethania.TVV 296.2

    Kule kukawia kwake kwa siku mbili wanafunzi wake walidhani kuwa amepuuza habari hizo. Wanafunzi walifikiri habari za Yohana Mbatizaji. Kwa nini Yesu hakumtoa gerezani wala kumfufua na hali alikuwa na uwezo wa kutenda miujiza? Mafarisayo walileta hoja hiyo, kama kanusho la kujidai kuwa Mwana wa Mungu. Kristo alikuwa amewaonya wanafunzi kuhusu majaribu, kupotea, na mateso. Je, atawaacha majaribuni? Mambo haya yote yaliwahangaisha mioyoni.TVV 296.3

    Baada ya kungoja siku mbili, Yesu alisema: “Twendeni huko Uyahudi tena.” Hawakuweza kuona kitu kingine, ila hatari tu. Walisema: “Bwana, juzijuzi Wayahudi walitaka kukupiga kwa mawe, nawe unataka kwenda huko tena?” Yesu akajibu na kusema, “Mchana hauna saa kumi na mbili? Mimi niko kwenye ulinzi wa Baba. Kadiri ninavyotenda mapenzi yake, maisha yangu yako salama. Nimefikia mwisho wa siku zangu, lakini wakati uliobaki niko salama.’ “Mtu akitembea mchana hajikwai, kwa kuwa kuna nuru ya mchana.” Mchana hajikwai, kwa kuwa kuna nuru ya mchana. Nuru ya uongozi wa Mungu humpa uhakika wa kazi yake. Nayo humwongoza mpaka mwisho wa kazi yake. Lakini mtu akitembea gizani hujikwaa kwa kuwa hakuna nuru ndani yake. Mtu atembeaye kama apendavyo hujikwaa. Maana hakuna usalama katika kutembea kama mtu apendavyo.TVV 296.4

    “Maneno haya aliyasema Yesu, baadaye aliwaambia, rafiki yetu Lazaro amelala, nami ninakwenda nipate kumwamsha.” Kuhusu hatari Bwana wao alipaswa kwenda Yerusalemu. Wanafunzi walikuwa karibu kusahau kuhusu maafa ya Bethania, lakini Kristo hakusahau. Wanafunzi walikuwa wameshasahau juu ya fadhili Mwokozi alizokuwa nazo kuhusu Lazaro na dada zake. Lakini ahposema rafiki yetu Lazaro amelala, ndipo walishituka na kukumbuka mambo yalivyo. Kristo hakuwasahau rafiki zake.TVV 297.1

    Kisha wanafunzi wake wakasema: “Bwana, kama amelala, ataamka. Walakini Yesu alisema habari za kufa kwake. Wao walidhani kuwa anasema juu ya kulala usingizi.”TVV 297.2

    Yesu alifananisha kifo na kulala usingizi, kwa waaminifu wake. Maisha yao yamefichika ndani yake katika Mungu. Na katika siku ya mwisho tarumbeta itawaamsha wote waliolala ndani yake. Tazama 1 Wakorintho 15:51-54.TVV 297.3

    Kisha Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa. Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako, ili ninyi mpate kuamini, walakini twende huko.”TVV 297.4

    Wanafunzi walishangaa kwa maneno ya Kristo, kwamba: “Lazaro amekufa, Nami nafurahi . . . sikuwako huko.” Je, Mwokozi alikosa kwenda kwa mgonjwa kwa mapenzi yake mwenyewe? Lakini Kristo aliona mpango wote, na kuwaona wale dada wenye kulia watafarijika kwake. Yesu aliona masikitiko yote ya hawa madada kwa ajili ya kifo hiki. Lakini Kristo hakuwafikiria watu wa jamaa hiyo tu katika Bethania. Aliwafikiria wanafunzi wake pia waliokuwa mafunzoni. Watakuwa wajumbe wake ulimwenguni. Kwa ajili yao Lazaro aliruhusiwa afe. Kama ungaliponywa ugonjwa tu, mwujiza muhimu ambao ni uthibifisho kamili wa Uungu wake usingelifanyika.TVV 297.5

    Kama Kristo angalimkuta mgonjwa, kifo kisingalimpata. Hiyo ndiyo sababu ya Yesu kutokuwako. Aliwaacha wale madada wamwone kaka yao akifa. Aliwaacha wavumilie huzuni yote bila kubakiza. Alijua kuwa Lazaro atafufuka sio kwa uwezo wake.TVV 297.6

    Kwa wote watakaotegemea uongozi wa Mungu, wakati wa huzuni kuu, ndipo wataona kuwa msaada na faraja iko karibu sana. Wataangalia nyuma wakati wa giza kuu kwa shukrani wakiona wakati ule wa giza. Kwa kila jaribu na shida atawatoa na kuwaleta katika hali ya utulivu na furaha tele, hali wakiwa na uthabiti na imani kamili.TVV 297.7

    Kristo alikawia ili kwa kumfufua Lazaro, apate kuwapa watu hawa wagumu na wasioamini uthibitisho kuwa hakika huyu ni “ufufuo na uzima”. Alitaka kuwapa watu hawa wasioamini, uhakika kuwa, yeye ndiye peke yake aletaye uzima na tumaini la Waisraeli. Ndiye asili ya uzima na nuru. Ndiyo sababu ya kukawia kwake.TVV 298.1

    Alipofika Bethania, Yesu aliwajulisha madada wale kwamba amekuja, lakini alibaki huko njiani muda kidogo. Kundi kubwa la waombolezaji kwa ajili ya kifo cha jamaa, hali kuafikiana na mipango ya Kristo. Alisikia maombolezo kwa mbali, naye hakutaka akutane na dada wale katika ghasia za jinsi hiyo. Katika baadhi ya waombolezaji, walikuwa maadui wa Kristo. Alijua kusudi lao, kwa hiyo hakutaka kukutana nao mara moja.TVV 298.2

    Martha alipashwa habari kimya kimya, watu wasisikie, hata Mariamu pia hakujua. Moyo wa Martha ulijaa huzuni. Alipofika kwa Kristo aliona huzuni ile ile vile vile, ila alimfikiria marehemu, na kusema: “Bwana kama ungalikuwa hapa ndugu yangu asingakufa.” Dada huyu alirudia maneno haya tena na tena.TVV 298.3

    Martha hakuwa na mashaka juu ya kurudia mambo ya nyuma, lakini alipomwangalia uso wake wenye huruma alisema:” Najua kuwa lolote utakalo mwomba Mungu atakufanyia.” Yesu alimfariji akisema: Ndugu yako ataishi.” Jibu hilo lilimfikirisha Martha juu ya ufufuo wa mwisho. Martha akasema: “Najua kuwa atafufuka siku ya mwisho.” Yesu akitaka kumhakikishia, alisema: “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima.” Katika Kristo ndipo asili ya uzima ulipo. “Aliye naye Mwana anao uzima.” 1 Yohana 5:12. “Aniaminiye mimi, ijapokuwa amekufa, ataishi, naye mwenye kuishi, akiamini hatakufa. Je, wayaamini haya?” Hapa Kristo anaangalia wakati wa kurudi kwake. Wakati wa kurudi kwake wafu walio mwamini watafufuka, na walio hai watabadilika bila kuonja mauti. Kumfufua Lazaro kutakuwa mfano wa wenye haki waliokufa watakaofufuliwa. Kwa maneno na kazi za Yesu humfanya kuwa asili ya kuwapa watu uzima wa milele.TVV 298.4

    Maneno ya Mwokozi, kwamba: “Waamini?” Martha alijibu “Ndiyo Bwana, naamini kuwa wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu, atakayekuja ulimwenguni.” Alikiri kuwa na imani kuhusu Uungu, na kuhusu uwezo wa kutenda apendavyo.TVV 298.5

    Alipokwisha kusema hivyo, aliondoka, akamwita dada yake Mariamu kisirisiri, akisema: “Bwana amekuja.” Alisema polepole iwezekanavyo, maana Makuhani na wakuu walipanga kumkamata Yesu ikiwezekana. Kilio cha waombolezaji kiliwazuia wasisikie maneno yake.TVV 298.6

    Mariamu aliposikia aliondoka mara moja akaenda. Waombolezaji walimfuata wakidhani kuwa anakwenda kaburini. Alipomfikia Yesu alisema, kwa masikitiko: “Bwana kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu asingalikufa.” Vilio vya waombolezaji vilimwumiza, naye alitaka kusikia maneno ya faraja kidogo.TVV 299.1

    “Yesu alipomwona akilia, na Wayahudi pia wakilia pamoja naye, alihuzunika moyoni naye akalia.” Aliona wengi walikuwa wakijifanya tu kama wenye masikitiko. Baadhi ya waliokuwa wakijifanya, walikuwa na njama ya kuua. Yesu aliuliza: “Mmemweka wapi?” Wakasema: “Bwana, njoo uone.” Wakaenda wote pamoja kaburini. Lazaro alikuwa mpendwa sana, na dada zake walimlilia kwa uchungu mno, na wengineo walijiunga na Mwana wa Mungu alikuwa amechukua mwili wa kibinadamu, ndiyo sababu alipata masikitiko kama wao.TVV 299.2

    Yesu hakulia kwa sababu ya Martha na Mariamu, bali alilia kwa sababu ya masikitiko ya miaka yote ya binadamu yalikuwa juu yake. Aliona matokeo mabaya mno ya kuvunja sheria ya Mungu. Aliona kuwa mapambano ya haki na uovu yameongezeka zaidi na zaidi. Aliona masikitiko na vifo, ambavyo vingalikuwa mzigo wa watu wote siku zote. Ole wa wanadamu wenye dhambi wote ulikuwa unamkalia yeye, kwa hiyo machozi yake yalitoka kwa kuwahurumia.TVV 299.3

    Lazaro alikuwa amewekwa kaburini, na jiwe kubwa sana lilikuwa limewekwa mlangoni. Kristo alisema: “Liondoeni jiwe.’ Martha alikanusha, kwa kudhani kuwa Yesu anataka kuona alikolazwa. Alisema kuwa ananuka sasa kwa kuwa tangu kuzikwa sasa ni siku nne. Usemi huu, haukuwapa nafasi maadui zake kupenyeza hoja zao za kusema kuwa kuna udanganyifu uliofanyika. Kristo alipomfufua binti Yairo, alisema: “Msichana hakufa bali analala’” Marko 5:39. Kwa vile alivyofufuliwa mara moja, Mafarisayo walikanusha kwa kusema kwamba binti alikuwa hakufa, ila amelala. Walijaribu kusema kuwa hakuna mwujiza uliofanyika, ila ni udanganyifu tu. Lakini kwa habari za kufa kwa Lazaro hakuna mtu angalikanusha, kwa kuwa amekuwa kaburini siku nne.TVV 299.4

    Bwana anapokuwa tayari kufanya kazi yake, Shetani humwinua mtu fulani kupinga. Martha alipinga kwamba mwili umeoza sasa. Maneno yake hayakulingana na ukweli aliouamini, wa ahadi ya ufufuo. Mwokozi alimsahihisha Martha kwa kusema: “Sikukuambia kwamba ukiamini utaona utukufu wa Bwana?” Unalo neno langu wala hakuna kitakacholipinga, na kuzuia kazi za Mwenyezi. Kutokuamini sio unyenyekevu, bali kuamini neno la Kristo ndio unyenyekevu na kujitoa kwa kweli. “Liondoeni jiwe.” Kristo angaliweza kuwaagiza malaika waliokuwa wakiwazunguka kufanya hivyo, lakini alitaka wanadamu kushirikiana na wanadamu. Kile watu wanachoweza kufanya Mungu huwaacha wafanye. Wasichoweza, ndipo Mungu huingilia.TVV 299.5

    Amri hiyo ilitiiwa. Jiwe liliondolewa. Kila kitu kilifanyika waziwazi. Wote waliona kuwa hakuna udanganyifu. Pale mwili wa Lazaro ulikuwa umelala, amekufa. Watu waliokuwako walingoja kwa hamu kitakachofuata. Watu walikuwa kimya. Kristo alisogea karibu na kaburi. Kristo akiinua macho yake mbinguni, alisema, “Baba, nakushukuru, kwa kuwa unanisikia.” Adui za Kristo wamemshutumu, kwamba anakufuru na kujiita Mwana wa Mungu.TVV 300.1

    Kristo alijihadhari asifanye jambo kisirisiri, ila wazi. Alimtegemea Baba yake kabisa. Ni kwa imani na kwa maombi ndiyo aliweza kufanya miujiza. Alitaka watu wote wafahamu uhusiano wake na Baba yake. Kwa hiyo alisema: “Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nimejua ya kuwa hunisikia siku zote, lakini kwa ajili ya watu hawa nasema hayo, ili wapate kuamini kuwa ni Wewe uliyemtuma.” Wanafunzi wake na watu wengine walijua ya kwamba madai ya Kristo siyo ya uongo.TVV 300.2

    Alipokwisha kusema hayo, alisema kwa sauti kuu: “Lazaro toka nje.” Uungu ulimulika katika ubinadamu. Katika uso wake uliong’aa kwa utukufu wa Mungu, watu waliona uthibitisho wa uwezo wake. Kila mtu alitazama kaburini, kila sikio liliinama kusikia chochote. Wote walisikiliza kwa hamu sana, kuona madai ya Yesu kuwa Mwana wa Mungu yalivyo.TVV 300.3

    Kulikuwa na kujongezana kaburini, ndipo aliyekuwa amekufa alisimama mlangoni. Mwendo wake ulizuiwa na sanda alizofungwa. Kwa hiyo Kristo aliwaambia wenye kushangaa “Mfungueni sanda.” Tena alionyesha kuwa binadamu ahudumie binadamu. Lazaro akasimama mbele ya wote, akiwa hana alama ya mauti. Mtu mzima kabisa. Macho yake yaling’aa kama kawaida, akampenda mponya wake sana na kumsujudia.TVV 300.4

    Watu walinyamaza kimya mara ya kwanza, kwa mshangao mkubwa. Halafu furaha ikafuatia na vifijo vyote. Madada zake wakampokea kaka yao kama zawadi kutoka kwa Mungu. Wakamshukuru Mwokozi kwa machozi ya furaha isiyosemaka. Wakati wa hoihoi za furaha, Yesu alitoweka. Walipomtafuta mwenye uzima hawakumwona.TVV 300.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents