Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kielelezo kwa akina Mama na Baba

  Watoto ni wepesi sana kufundishwa injili, mioyo yao hupokea mafundiso kwa upesi sana. Watoto waweza kuwa wakristo kufuatana na umri wao. Wazazi wangehesabu watoto wao kuwa ni washiriki wao katika jamaa, wakiwaongoza kuelekea mbinguni. Nyumba ya kikristo ingekuwa shule ya kufundisha, wazazi wakiwa walimu wadogo, na Kristo akiwa mwalimu mkuu. Yatupasa kuwafundisha watoto wetu kuleta dhambi zao kwa Kristo, wakimwomba awasamehe, hali wakiamini kuwa watasamehewa na kupokelewa, kama alivyowapokea watoto zamani.TVV 289.3

  Jinsi mama anavyomfundisha mtoto wake kumtii, maana anampenda, huwa anamfundisha fundisho la kwanza la maisha katika ulimwengu. Upendo wa mama kwa mtoto wake huwa mfano wa upendo wa Kristo, na mtoto anavyojifunza kumtii na kumheshimu mama, huwa anajifunza kumtii Kristo, ambaye ni Mwokozi wake.TVV 289.4

  Yesu pia alikuwa kielelezo cha Baba. Maneno yake yalikuwa na uwezo, hata watu wakorofi, walimtii bila kutumia maneno makali. Neema katika maneno ya Kristo iliwalainisha hata watu wakaidi. Maneno hayo yatawafunza akina mama na baba kuwasamehe watoto wao kama wao wenyewe wanavyopenda kusamehewa.TVV 289.5

  Wazazi, katika kazi ya kuwafundisha watoto wenu, jifunzeni jinsi Mungu alivyosema kuhusu mambo ya asili, jinsi anavyofanya kwa viumbe. Kama mngezoeza maua ya waridi, mngefanyaje? Mwulize mtunza bustani akueleze namna anavyoyaongoza maua yaendelee kuslawi na kupendeza. Atakuambia kuwa, siko kuyashika kwa nguvu na kuyayumbishayumbisha wala siyo kuyavurumisha huku na huko kutakakoyasaidia kuendelea vema na kupendeza, ila ni kutenda kidogo kidogo, na kurudia mara kwa mara, na kuyasamadi na kuyang’olea kwa taratibu magugu, na kuyashika kwa polepole. Kufundisha kwa upole, ndivyo utaweza kuongoza tabia zao kuelekea katika tabia ya Kristo.TVV 289.6

  Watie moyo kusema msemo wa upole na wema kumhusu Mungu na kusemezana wao kwa wao. Sababu ya kuwa na wakorofi wengi uliniwenguni leo ni kwa kuwa misemo ya upendo na fadhili imetoweka sana kwa watu. Mianzo ya watu hawa iliharibiwa na kufanywa migumu katika utoto wao. Upendo wa Mungu usipoingilia kati, maisha yao yataharibika kabisa. Kama tukitaka watoto wetu wawe na hali ya fadhili kama ya Yesu, yatupasa kukuza hali ya wema, ukarimu, upole na wema katika maisha yao ya tangu utoto.TVV 290.1

  Wafundishe watoto kujifunza na kumwona Yesu katika viumbe. Wachukue waende huko katika miti ya milima, na maua. Katika viumbe vyote vya asili, wafunze kumwona Yesu anavyotenda kwa fadhili. Hufanya sheria inayoongoza viumbe vilivyo hai. Naye amefanya sheria inayotuletea faida na furaha. Usiwasumbue na sala ndefu na mambo mengi, ila waelekeze kumtii Mungu na sheria yake.TVV 290.2

  Wakati unapojaribu kupanga ukweli wa wokovu, waelekeze watoto kwa Kristo aliye Mwokozi wa kila mtu peke yake. Malaika watakuzunguka ili kukusaidia. Mungu atawapa akina baba na mama neema ya kuwawezesha kuwaelekeza watoto wao kwa mtoto wa Bethlehemu.TVV 290.3

  Usiwapeleke watoto mbali na Yesu, kwa njia ya mambo ya ufisadi na ukorofi. Usiwafanye waone kuwa mbingu itakuwa mahali pabaya pa kuishi kama na wewe utafika, huko pia. Usiseme juu ya dini kana kwamba watoto hawawezi kuifahamu. Usiwakoseshe watoto kwa kudhani kuwa mbinguni ni mahali pasipokuwa na furaha, ila ni mahali pa ukiwa tu, na kudhani kuwa kumfuata Kristo ni kuacha kila kitu.TVV 290.4

  Roho Mtakatifu anapowavuvia watoto shirikiana nao katika kazi yao. Mwokozi huwaita. Hakuna kitu kinachompendeza kuliko kuona watoto wakitoa kwake katika miaka yao ya utotoni. Roho yake huwafikia, si watoto wema tu, ila hata wale wenye tabia mbaya waliyorithi kwa kufundishwa vibaya. Wazazi wengi hawana hekima ya kuwalea watoto wao kama ipasavyo. Lakini Yesu huwaangalia watoto hawa kwa huruma.TVV 290.5

  Uwe mjumbe wa Kristo wa kuwalea watoto hawa kwake. Uwaelekeze kwa utaatibu na kwa hekima mpaka kwa Kristo. Kwa neema ya Yesu watabadilika katika hali yao, ili isemwe kwao maneno haya: “Watoto wa namna hii ufalme wa Mungu ni wao.”TVV 291.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents