Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mbingu zinapoanza

    “Amin, amin, nawaambieni, yeye aniaminiye ana uzima wa milele.” Huo ndio usemi wa Yesu. “Nami nitamfufua siku ya mwisho.” kristo alikuwa katika hali moja na sisi, katika mwili, ili sisi tuwe katika hali moja naye katika roho. Kwa njia ya mwungano huu wa uwezo, tunaweza kufufuka kutoka kaburini, maana kwa imani maisha yake yamekua maisha yetu. Wanaomwona Kristo na kumpokea mioyoni wanao uzima wa milele. Kwa njia ya Roho Kristo huishi ndani yetu; na Roho wa Mungu akipokelewa kwa imani, huanza uzima wa milele.TVV 214.1

    Mana ambayo ililiwa na baba zetu huko jangwani haikuweza kuzuia kifo, wala kuleta hali ya kutokufa kwa watu, lakini mkate wa mbinguni utawezesha mtu kuufikia uzima wa milele. Mwokozi alisema: “Huu ni mkate ushukao kutoka mbinguni, ili mtu akiula asife.” Kwa kifo cha Kristo tu ndipo watu watapata uzima. Alionyesha katika kifo chake kuwa ndipo penye ukombozi. “Chakula nitakachowapa ni mwili wangu nitakaotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”TVV 214.2

    Katika mfano wa kondoo wa pasaka, Wayahudi hawakuelewa mwili wa Bwana. Ukweli ule ule ulifundishwa kwa maneno ya Kristo, lakini haukufahamika hata hivyo. Sasa Marabi waliuliza, huku wakikasirika, “Anawezaje mtu huyu kutupa mwili wake tuule?” Walifahamu maneno ya Yesu, kwa sehemu fulani, lakini kwa jeuri tu walitumaini kuwakoroga watu wampinge Yesu.TVV 214.3

    Kristo aliikariri kweli kwa nguvu zaidi, akisema: “Amin, amin, nawaambieni, Msipokula mwili wa Mwana wa Adamu na kunywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Mtu atakayekula mwili wangu na kunywa damu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. Maana mwili wangu ni chakula cha kweli; na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Mtu yeyote aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu na mimi ndani yake.”TVV 214.4

    Chakula ni nini kwa mwili? Kristo lazima akae ndani ya mtu. Chakula hakitusaidii kitu kisipokuwa kinaingia ndani yetu na kuwa sehemu yetu. Hivyo basi kuwa na elimu juu ya dini na tarativu zake bila kuzitekeleza hakutufai loloe. Lazima tumle Kristo, maisha yake, upendo wake, neema yake lazima viwe sehemu yetu.TVV 214.5

    “Kama Ba ba alivyonituma, nami naishi kwa amri zake, ndivyo alivyo yeye aulaye mwili wangu, naye ataishi ndani yangu” Ndivyo yesu alivyojitoa kamili kwa mapenzi ya Baba, kwamba Baba peke yake ndiye alidhihirika katika maisha yake. Ingawa alijaribiwa katika mambo yote, kama sisi, lakini aliishi bila kutenda dhambi zilizomzunguka. Ndivyo hata sisi inatupasa kushinda kama Kristo alivyoshinda. Je, wewe ni mfuasi wa Kristo? Basi yote yaliyoandikwa kuhusu mambo ya kiroho ya yesu, yanaweza kuonekana ndani yako kwa ajili ya kuunganika naye. Je, upendo wako wa kwanza umepoa? Pokea tena upendo wa Kristo. Kula tena mwili wake na kuinywa damu yake; ndipo utakuwa mmojawao wa Baba na Mwana.TVV 215.1

    Kwa sheria Wayahudi walikatazwa kuonja damu, na sasa wao wameelewa lugha ya Yesu juu ya mwili na damu. Wengi hata katika wanalunzi wake walisema kuwa neno hilo ni gumu. Nani ataliweza?TVV 215.2

    Mwokozi aliwajibu akisema, “Neno hili limewakwaza? Itakuwaje mtakapomwona Mwana wa Adamu akipanda kwenda huko alikokuwa hapo kwanza? Roho ndiyo itiayo uhai, mwili haufai kitu, neno ninalowaambia ni roho tena ni uzima”TVV 215.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents