Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    37 — Wainjilisti wa Kwanza

    Mitume walifuatana na Yesu wakitembea kwa miguu katika nchi yote ya Galilaya. Walikuwa wakiongea na kufanya kazi pamoja na Mwana wa Mungu, huku wakijizoeza jinsi ya kuwahudumia wanadamu. Yesu alipokuwa akiwashughulikia mkutano, wanafunzi nao walikuwa wakisaidia kumpunguzia Yesu mzigo wa kazi. Waliwasaidia walemavu kuwaleta kwa Yesu, na kuwafariji wote. Waliona watu wenye kupenda maneno ya Mungu, na wakawasaidia kutatua matatizo waliyokuwa nayo kuhusu maandiko matakatifu.TVV 192.1

    Walakini walihitaji mazoea ya kufanya kazi peke yao. Pia walihitaji mafundisho zaidi kutoka kwa Yesu. Sasa badala ya kukaa pamoja nao na kuwaongoza katika mambo mbalimbali, Yesu aliwatuma ili wakajizoeze kufanya kazi peke yao kama wajumbe wa Injili.TVV 192.2

    Kila mara wanafunzi waliona matatizo ya kukabiliana na Mafarisayo na makuhani, wakati walipowafundisha, na mara nyingi walimletea Yesu matatizo hayo. Yesu alikuwa amewaimarisha katika neno la Mungu, na alikuwa amewaweka mbali na mambo ya mapokeo yasiyokuwa na msingi. Alipowatenga mbali na yeye iliwapasa kujitegemea katika mambo yote, wakisimama katika ukweli wa neno la Mungu peke yake.TVV 192.3

    Aliwatuma waende katika miji yote, wakiwa wawili wawili. Hivyo walitiana nguvu na kuomba pamoja katika mambo yote.TVV 192.4

    Kazi ya Uinjilisti ingefaulu zaidi kama mpango huu ungalifuatwa.TVV 192.5

    Wanafunzi hawakupaswa kuingia katika mabishano kwamba Yesu ni Masihi, au la. Lakini kwa jina lake wataponya wagonjwa, watatakasa wenye ukoma, watafufua wafu, watafukuza pepo. Waliagizwa: “Mmepata bure, toeni bure.”TVV 192.6

    Yesu alitumia wakati mwingi kuponya awagonjwa kuliko kuhubiri. Popote alipoenda furaha yake ilikuwa afya. Sauti yake ndiyo iliyotakiwa kusikiwa zaidi ya yote. Jina lake ndilo lililotakiwa ulimwenguni Uso wake ndio uliofurahiwa zaidi. Alipokuwa akipita katika miji na vijijini alikuwa sawa na mkondo wa maji yenye kuleta furaha na uhai.TVV 193.1

    Wafuasi wa Kristo wapaswa kufanya kama vile yeye alivyofanya. Inatupasa kuwalisha wenye njaa, kuwafariji wenye dhiki, na kuwapa matumaini wale wasiokuwa na matumaini. Upendo wa Kristo ukionekana katika kazi yetu isiyokuwa na ubinafsi, itafaulu kabisa kuwaongoa wenye dhambi kuliko upanga, au mahakama ya hakimu yanavyoweza kufanya. Roho zitakuwa tayari chini ya upendo wa kikristo kuliko kitu kinginecho. Mungu anataka kuwa Mfariji Mkuu kwa watu kwa njia ya watumishi wake; ili ulimwengu uone upya ambavyo haujaona hivyo.TVV 193.2

    Katika safari ya kwanza ya wanafunzi kwenda kama wahubiri, walikwenda kwa “Kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” Kama wayahudi wanagalilipokea neno la Mungu, angaliwafanya kuwa wajumbe wake kati ya watu wa mataifa. Kwa hiyo wao ndio walikuwa watu wa kwanza kupelekewa ujumbe huu.TVV 193.3

    Katika safari hii ya kwanza wanafunzi walikwenda pale ambapo Yesu alikuwa ameshafika; na kufanya urafiki na watu. Kwa hiyo matayarisho kwa safari hiyo yalikuwa rahisi tu. Hawakupaswa kuwa na mavazi raswmi yanayovaliwa na walimu wa dini, wala hawakupaswa kuwa na mavazi ya pekee ya kuwapambanua kati ya watu wa kawaida. Wala haikuwapsa kukusanya watu kwa ajili ya mikutano yao. Kazi yao ilikuwa kuingia nyumba kwa nyumba. Kila mahali iliwapasa kupokea makaribisho ya wenyeji kama Kristo angalikuwako na kukubali. Watatoa salamu ya kawaida inayotolewa kwamba.” . . . Amani iwemo nyumbani humu.” Luka 10:5. Nyumba hii itabarikiwa kwa njia ya maombi, na nyimbo zao za kusifu, pamoja na kufungua neno la Mungu na kulisoma humo. Ujumbe wao, ambao watauchukua ni neno la uzima, na matokeo ya watu wa nyumba hiyo, hutegemea kulipokea au kulikataa neno hilo. Soma Mathayo 10:14, 15.TVV 193.4

    Yesu alisema: “Angalieni nawatuma kama kondoo kati ya mbwa wa mwiatu; kwa hiyo iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.” Kristo hakuondoa hata neno moja la kweli, ila alisema neno la ukweli katika upendo. Hakuwa mkaidi hata kidogo; wala hakumkasirisha mtu yeyote. Hakuulaumu udhaifu wa mtu yeyote. Aliukemea unafiki na uovu bila kuogopa. Lakini alikemea uovu kwa machozi. Kila mtu alikuwa wa thamani kwaka.TVV 193.5

    Watumishi wa Kristo wanahitajika kumkaribia Mungu sana, wasije wakatoa maneno yasiyotakiwa wakati wanapokemea uovu, yakaleta madhara. Watumishi wa Mungu inawapasa kukaza macho yao kwa upendo wa Kristo. Ndipo atatoa injili kwa hekima ya Mungu. Roho ya mtu ambayo inahifadhika na kutunzwa kwa hekima itatoa maneno yenye busara, ambayo hayawezi kubishiwa.TVV 194.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents