Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    4 — Kuzaliwa Zizini

    Mfalme wa utukufu alishuka chini sana ili kuwa mwanadamu. Utukufu wake ulifunikwa kabisa bila kuonekana. Yesu alikusudia kwamba, pasiwepo kitu chochote kwake chenye kuwavutia watu, ili wamwendee. Watu wenye kumfuata wavutwe kwake na usafi na ukweli wa ujumbe wa Injili tu. Alitaka watu wamwamini kwa ushahidi wa neno la Mungu peke yake.TVV 21.1

    Malaika waliangalia ili waone jinsi watu wa Mung wampokeavyo Mwana wake; aliye na hali ya ubinadamu. Katika nchi ambapo nuru ya unabii imeng’aa malaika wlaikuja. Walikuja bila kuonekana katika Yerusalemi, na kuhudumu katika nyumba ya Mungu.TVV 21.2

    Kuja kwa Kristo kulikuwa kumetangazwa kwa Zekaria, aliyekuwa nabii akihudumu katika madhabahu. Tayari mtangulizi wa Kristo alikuwa amezaliwa, na habari za kuzaliwa kwake na kazi yake ilikuwa imetangazwa. Walakini Yerusalemi haikuwa na habari, wala haikuwa tayari kumpokea Mkombozi. Mungu aliwaita Wayahudi wapate kueneza habari za kuja kwa kristo, kwamba atazaliwa katika mlango wa Daudi, walakini hawakuwa na habari kwamba kuja kwake kumekaribia.TVV 21.3

    Katika hekalu dhabihu zilizokuwa zikitolewa asubuhi na jioni, zilielekeza juu ya Mwana-kondoo wa Mungu, hata hivyo hakuna matayarisho yoyote yaliyofanywa kwa kumpokea. Makuhani na walimu, walikariri sala, ambazo hazina maana yoyote kila siku, na kufanya huduma na kushika kawaida za ibada, lakini bila kutayarisha matokeo ya kuzaliwa Kristo. Hali ya usingizi ile ile ilifunika nchi nzima ya Israeli. Hali ya ubinafsi na kushughulikia mambo ya ulimwengu, vilifunga miyo ya watu wasiweze kusikia furaha iliyokuwa ikifurahiwa na mbingu. Watu wachache tu walitamani kuona mambo yasiyoonekana.TVV 21.4

    Malaika walifuatana na Yusufu na Mariamu katika safari ya kutoka Nazareth kwenda katika mji wa Daudi. Amri ya Rumi ya kuwaandikisha watu wote ilikuwa imetangazwa katika dola yake yote mpaka Galilaya. Mfalme Augustus akakwa mjumbe wa Mungu kumleta mama wa Yesu huko Bethlehemu. Alikuwa wa ukoo wa Daudi; na Mwana wa Daudi lazima azaliwe katika mji wa Daudi. Nabii alisema, “Kwako (Bethlehemu), atakuja . . . mtawala wa Israeli; ambaye kwenda kwake kumekuwa tangu zamani za kale tangu milele.” Mika 5:2.TVV 22.1

    Lakini katiia mji huu wa utawala, Yusufu na Mariamu hawakujulikana, wala kujali wa na mtu. Wakiwa wamechoka, na hawana mahali pa kukaribishwa, Yusufu na mkewe walijikokota wakipita katika njia nyembamba mpaka upande wa mwisho wa mji huko mashariki, wasione mahali pa kulala usiku. katika nyumba ya wageni hapakuwako nafasi. Katika banda la wanyama ndipo wlaipata nafasi baada ya kuhangaika sana. Na hapo ndipo Mwokozi alizaliwa.TVV 22.2

    Habari hii iliifurahisha mbingu mno. Watakatifu kutoka katika dunia zisizoanguka walivutwa kuja katika dunia yetu. Katika vilima vya Bethlehemu lilikuja jeshi la malaika. Lilikuwa linangoja ishara ili lipate kutangaza habari hii ya kuzaliwa kwa Masihi katika ulimwengu.TVV 22.3

    Waongozi wa Israeli wangalijiunga katika furaha hii pia. Lakini walipitwa bila habari yoyote. Wale waliokuwa wakitafuta nuru na kuiamini kwa furaha, nuru ya urukufu kutoka kaika kiti cha enzi cha Mungu iliwang’aria. Soma Isaya 44:3; Zaburi 112:4.TVV 22.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents