Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kielelezo cha Kristo, hukataza kutenga

    Ni kweli kwamba dhambi ya dhahiri humzuia mtu asishiriki katika meza ya Bwana. (Tazama 1 Wakorintho 5: 11.) Lakini zaidi ya hayo hakuna awezaye kuhukumu. Ni nani awezaye kusoma siri za moyo, au kubagua kati ya magugu na ngano? “Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.” “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.” “Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupa-rnbanua ule mwili.” 1 Wakorintho 11: 28, 29.TVV 372.4

    Wakati waumini wanapokutana kuadhimisha ibada hizi za dini, kunawezekana kuwamo akina Yuda pia, katika kundi kama ndivyo, wajumbe wa mwovu huwamo vile vile, maana huja kuwaunga mkono wale wote wanaokataa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Malaika wa mbinguni pia huwapo. Hapo wanaweza kuwapo watu ambao si watumishi wa kweli na utakatifu, lakini wanaopenda kushiriki huduma hiyo. Watu kama hao wasizuiwe. Ma-shahidi wako hapo kama walivyokuwako wakati Yesu akitawadha miguu ya wanafunzi.TVV 373.1

    Kristo huwapo kwa njia ya Roho Mtakatifu, ili kusadikisha na kulainisha moyo. Hakuna hata wazo moja la toba linatoka pasipo kulifahamu. Anawangoja wenye toba na mioyo iliyovunjika. Yeye aliyeosha miguu ya Yuda hutamani kutakasa kila moyo kutokana na doa la dhambi.TVV 373.2

    Watu wo wote wale wasijitenge wenyewe kutoka katika ushirika wa meza ya Bwana, kwa sababu eti wapo watu wasiostahili kuwapo. Katika mikutano hii, mikutano yake mwenyewe Kristo hukutana na watu wake na kuwatia nguvu kwa kuwako kwake. Mioyo na mikono isiyostahili inaweza hata kuhudumia katika huduma hii, hata hivyo wale wanaokuja wakiwa na imani iliyokazwa juu ya Kristo wataabarikiwa mno. Wote watakaodharau maadhimisho haya, watapata hasara ya kupotea. Huduma ya meza ya Bwana ilikusudiwa kudumisha mbele ya wanafunzi dhabihu isiyo na kikomo iliyotolewa kwa kila mmoja wao binafsi, kama sehemu ya wanadamu wote walioanguka.TVV 373.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents