Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hakuna msururu wa maombolezo katika ushindi huu

    Kamwe ulimwengu ulikuwa haujapata kuona maandamano ya ushindi jinsi hii. Mwokozi alizungukwa na nyara tukufu za kazi zake za upendo kwa mwanadamu mwenye dhambi. Hizi zilikuwa mateka waliokolewa kutoka kwa mamlaka ya Shetani. Vipofu waliokuwa wamepata kuona waliongoza maandamano. Bubu waliokuwa na ndimi huru walipiga kelele za Hosana. Viwete waliokuwa wameponywa nao waliruka ruka kwa furaha. Wenye ukoma aliowatakasa walitandika mavazi yaliyosafi katika njia yake. Lazaro aliyeamshwa kutoka katika usmgizi wa mauti alimuongoza punda aliyepandwa na Mwokozi.TVV 321.2

    Mafarisayo wengi wakiwaka kwa hasira ya wivu, walijaribu kuwanyamazisha watu, lakini vitisho vyao viliongeza tu kelele za hoihoi. Katika juhudi ya mwisho walimwambia Mwokozi: “Bwana wanyamazishe watu hawa. Wanapiga kelele na kuvuruga mambo ambavyo si sheria.” Lakini Mafarisayo walinyamazishwa na jibu la Yesu, aliposema: “Nawaambieni, watu hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele mara moja.” Shangilio hili shangwe yalikuwa yametabiriwa na manabii. Watu wangeshindwa kutimiza mpango wa Mungu, mawe ambayo hayazungumzi, yangemshangilia Mwana wake. Mafarisayo waliponyamazishwa watu wakayatimiza maneno ya nabii Zekaria wakiimba:TVV 321.3

    Furahi sana, Ee binti Sayuni;
    Piga kelele, Ee binti Yerusalemu;
    Tazama, mfalme wako anakuja kwako;
    Ni mwenye haki, naye ana wokovu;
    Ni mnyenyekevu, amepanda punda,
    Naam, mwanap-unda, mtoto wa punda.
    TVV 321.4

    Maandamano yalipofika kwenye ukingo wa kilima, Yesu na maandamano yote walisimama. Mbele yao mji wa Yerusalemu ulitanda na utukufu wake, uking’aa kwa mwangaza wa jua kuchwa. Hekalu maarufu liliinuka kuliko majengo yote, ambalo lilikuwa fahari na utukufu wa taifa la Wayahudi. Hata Warumi pia walijivunia fahari yake. Fahari yake na utajiri wake vililifanya kuwa ni mojawapo ya maajabu ya ulimwengu.TVV 321.5

    Wakati jua lilipokuwa likishuka upande wa magharibi, miali yake ilipiga katika mawe ya hekalu yenye thamani kuu, na kuling’aza. Kutoka pale Yesu alipokuwa akisimama, lilionekana likimetameta kama jengo la barafu, lenye minara ya dhahabu, liking’aa kwa utukufu kana kwamba ni utukufu wa mbinguni.TVV 322.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents