Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Usikizi wa Mwanamke Umeamshwa

    Hali ya mwanamke ikaanza kubadilika kiusemi, akasema: “Bwana, huna kitu cha kuchotea maji, na hali kisima ni kirefu sana; nawe umepata wapi maji yaliyo hai? Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye alikunywa maji haya?” Mbele yake mwanamke huyu alimwona na kumfikiri msafiri huyu mchovu tu, anayetaka maji. Mwanamke huyu alimfananisha Yesu na Yakobo. Alikuwa akifikiria nyuma juu ya baba zake, na kumtazama Masihi ajaye, kumbe Masihi mwenyewe alikuwa pamoja naye, wala hakumjua. Watu wangapi leo walio na kiu ya haki huwa karibu na chemchemi, huku wakitafuta kwa mbali wapate kisima cha uzima!TVV 98.2

    Yesu alisema kwa makini: “Anywaye haya huona kiu tena: bali atakayekunywa maji nitakayompa hataona kiu kabisa: lakini maji nitakayompa yatakuwa chemchemi ibubujikayo hata uzima wa milele.”TVV 98.3

    Kila mahali watu hutafuta kitu kitakachowaridhisha katika haja zao. Mtu mmoja tu awezaye kuridhisha kila mwenye haja, yaaniknsto. Yeyendiye “Tunu ya mataifa yote.” Neema ya Mungu anayoitoa ni kama maji yenye uhai, yatakasayo, na kuimarisha mtu.TVV 98.4

    Yesu hakusema kuwa kila mtu achotaye maji haya tu ataridhishwa haja yake. Yule atakayeonja upendo wa Yesu atazidi kuutaka zaidi, wala hatataka kitu kingine zaidi. Utajiri, cheo na anasa za dunia havitamvutia kamwe. Kilio chake cha daima kitakuwa zaidi kwa Bwana. Mwokozi wetu ni chemchemi isiyokauka. Tunaweza kunywa kwake zaidi na zaidi bila upungufu wowote.TVV 98.5

    Yesu alikuwa ameamsha usikizi wa mwanamke huyu na shauku yake kwa kipawa alichotaka. Akasema, “Bwana, nipe maji hayo, ili nisione kiu tena, wala nisije hapa kuchota maji.”TVV 98.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents