Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kristo Afa Kifo cha Ushindi

  Ghafla giza lilitoweka msalabani. Na kwa sauti kama ya tarumbeta ambayo ilisikika kuvuma ulimwenguni kote, Yesu akapaza sauti, “Imekwisha.” “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Nuru ikauzingira msalaba, na uso wa Mwokozi ukang’aa kwa utukufu kama jua. Kisha akainamisha kichwa chake akakata roho. Katikati ya giza hilo la kutisha, Kristo alikuwa amekunywa mashudu yote katika kikombe cha msiba wa wanadamu. Katika saa hizo za kutisha alikuwa ametegemea ushuhuda wa kukubalika na Baba yake uliokuwa umetolewa kwake hapo awali. Akiwa anaifahamu tabia ya Baba yake, kwa imani alimtumaini yeye ambaye ilikuwa daima furaha yake kumtii. Na kadiri alivyojitoa kwa Mungu, ile hali ya kupoteza upendeleo wa Baba yake ilitoweka. Kwa imani, Kristo alikuwa mshindi.TVV 428.3

  Tena giza likaifunika nchi, na kukatukia tetemeko kuu la nchi. Kukawa na wasiwasi. Katika milima ya karibu miamba ilipasuka mapande na kuviringika mabondeni. Makaburi yalifunguliwa na wafu wakatupwa nje. Makuhani, askari, wanyongaji, na watu wote waliokuwapo hapo walianguka kifudifudi. Wakati sauti ya kilio “Imekwisha” iliposikika kutoka mdomoni mwa Kristo, ilikuwa ni wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. Kondoo anayemwakilisha Kristo alikuwa ameletwa kuchinjwa. Kuhani alisimama na kisu tayari hali watu wakiangalia.TVV 428.4

  Lakini nchi ilitetemeka kwa sababu Bwana Mwenyewe alikaribia karibu. Kwa sauti ya mpasuko, pazia la hekalu likapasuliwa kwa mkono usioonekana vipande viwili toka juu hata chini; na kukifungua wazi kwa macho ya watu chumba cha patakatifu pa patakatifu palipokuwa pakijaa utukufu wa Mungu. Mahali patakatifu mno pa hekalu la dunia hapakuwa patakatifu tena.TVV 429.1

  Kote kukawa na hofu kuu na kuchanganyikiwa. Kuhani alikuwa karibu kumchinja kondoo wa kafara; lakini kisu kilianguka kutoka mkononi mwa kuhani na yule kondoo akakimbia; Mfano ulikuwa umekutana na kilicho asili ya mfano. Sadaka kuu ilikuwa imetolewa. Sasa njia mpya na iliyo hai ilikuwa imetolewa kwa wote. Tangu sasa Mwokozi atahudumu kama kuhani na mtetezi katika mbingu za mbingu. “Kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata baada ya kupokea ukombozi wa milele” (kwa ajli yetu). Waebrania 9:12.TVV 429.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents