Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kabla ya Hukumu ya Mwisho

    Wakishikwa na hofu, makuhani na wakuu walikimbia kutoka hekaluni, wakiukimbia uso wa Yesu na macho yake yaliyoweza kusoma siri za mioyo yao. Katika hali hiyo Kristo aliona jinsi taifa zima la Wayahudi lilivyojitenga na Mungu kwa ajili ya uovu wao, na kutotubu kwao. Kwa nini makuhani walikimbia? Kwa nini hawakusimama? Aliyewaamrisha alikuwa mwana wa seremala, mtu wa Galilaya. Kwa nini hawakumpinga? Kwa nini waliacha faida zao wakakimbia nje kwa agizo lake yule aliyekuwa akionekana kuwa mtu wa kawaida tu?TVV 83.5

    Kristo alinena kwa mamlaka ya kifalme, na katika kuonekana kwake, na usemi wake, kulikuwako na uwezo ambao hawakuweza kuuvumilia. Katika maneno ya kuamuru waliona hali yao jinsi ilivyo hasa, yaani hali ya unafiki na unyang’anyi. Wakati Uungu ulipomulika katika ubinadamu; walifanana kama wako mbele ya hakimu, wakihukumiwa kifo cha milele. Kwa muda watu wengi walimwamini kuwa ndiye Masihi. Roho Mtakatifu aliwafunulia mioyoni mwao kuhusu usemi wa manabii juu ya Kristo je, watashikilia imani hiyo?TVV 84.1

    Hawakutubu. Walijua kuwa wamekuwa na hatia ya kutoza watu bure. Kwa kuwa Kristo aligundua siri zao, kwa hiyo walimchukia. Makemeo yake ya wazi mbele ya watu, yaliwaaibisha. Hivyo waliona wivu kwa jinsi alivyozidi kuwa na mvuto mkubwa. Walikusudia kukanushia mbali uwezo uliowafanya wakimbie.TVV 84.2

    Walirudi hekaluni polepole, huku wakiwa na chuki mioyoni mwao, wakatafakari sana juu ya haya yote. Wamepata badiliko kiasi gani! Walipokimbia, maskini walibaki nyuma, hekaluni, na hawa walikuwa wakimwangalia Yesu, ambaye uso wake ulikuwa na tabasamu na upendo.TVV 84.3

    Watu walisongamana kuja kwa Yesu, wakimwomba awabariki. Sikio lake lilisikia kila aina ya kilio au lalamiko. Kila mtu alisikilizwa. Kila mtu aliponywa maradhi yalikuwa yakimsumbua.TVV 84.4

    Makuhani na mkuu wa hekalu walipokuwa wakiangalia kazi kubwa hii, walipata mafunuo mapya kiasi gani. Watu walikuwa wakisimuliana maradhi waliyokuwa nayo, na jinsi walivyokuwa na matumaini ya bure, na jinsi walivyoishi kwa shida sana na masumbuko bure. Walipokata tamaa kabisa, Kristo aliwaponya wote. Mmoja alisema, “Lo, nilisumbuka sana, lakini nimepata msaidizi. Yeye ni Kristo Mwana wa Mungu, nitaandamana naye maisha yangu yote.” Wazazi walisema kwa watoto wao, “Ameokoa maisha yenu, msifuni yeye kwa shangwe.” Furaha na vicheko viliwajaza watoto, vijana, akina mama, na akina baba, na wote waliokuwa wakiangalia hayo. Walijazwa na furaha wakarudi nyumbani wakitangaza habari hizo; za upendo wa Yesu.TVV 84.5

    Wakati Yesu aliposulubishwa, watu walioponywa hawakujiunga na mkutano kumzomea, na kusema, “Msulubishe, msulubishe.” Wao walimsikitikia Yesu, maana wameona upendo wake wa ajabu, na uwezo wake. Walijua kuwa yeye ni Mwokozi wao. Waliwasikia mitume, nao wakawa wajumbe wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa watu.TVV 85.1

    Watu waliokimbia kutoka hekaluni, walirudi pole pole baadaye, lakini walikuwa na aibu kubwa. Waliamini kuwa unabii unaomhusu Masihi unakamilika kwa Yesu. Dhambi ya kuchafua hekalu ilikuwa kwa makuhani kwa sehemu kubwa. Kwa ajili ya mpango wao, uwanja wa hekalu uligeuka kuwa soko. Watu hawakuwa na hatia. Lakini makuhani na wakuu, walihesabu kazi ya Kristo kuwa ni mapinduzi ya sheria, wakamwuliza kuwa, ana haki gani kuingia katika mambo yaliyoruhusiwa na wenye mamlaka.TVV 85.2

    Walichukizwa kwa sababu ya kuingilia habari za biashara na kwa hiyo waliendelea kufanya shingo zao kuwa ngumu, wasijali mvuto wa Roho Mtakatifu.TVV 85.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents