Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wajibu wa Mchungaji Mwaminifu

    Katika upande wa Mashariki kazi ya uchungaji ilikuwa kazi ya daima na ambayo haikomi Wanyang’anyi au wanyama wakali walikuwa tayari kutawanya kundi la kondoo. Ulinzi wa mchungaji ulihitajika katika maisha yake yote. Yakobo aliyechunga makundi ya kondoo za Labani alisema: “Mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi, ukanitoka machoni mwangu.” Mwanzo 31:40. Kijana Daudi alipokuwa akilinda kondoo za Baba yake alikesha ili kuwalinda kondoo wasikamatwe na wanyama wa mwitu.TVV 272.3

    Mchungaji alijishughulisha na wale aliokabidhiwa. Kila kondoo alikuwa na jina lake, naye alimwitikia mchungaji. Ndivyo na Mchungaji anajua kondoo waliotawanyika ulimwenguni. Yesu alisema: ‘Nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.” Isaya 43:1. Yesu atujua kama tulivyo, kila mmoja wetu, na anajisikia kuwa na hali yetu ya udhaifu wetu. Anafahamu nyumba tunazoishi ndani yake. Wakati fulani amewaagiza watumishi wake kwenda katika nyumba fulani katika mji fulani ili kumtafuta kondoo wake aliyepotea.TVV 272.4

    Kila mtu anajulikana kwaYesu kana kwamba ndiye mwenyewe aliyefiwa na Yesu. Masikitiko ya kila mtu hugusa moyo wa Yesu. Alikuja kuwavuta watu wote kwake. Anajua mtu anayemsikia kwa furaha, na yuko tayari kuja chini ya ulinzi wake. Yeye husema: “Kondoo wangu husikia sauti yangu, nami nawajua, nao hunifuata.”TVV 272.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents