Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wengi walitamani Mkombozi

    Imani ya Wayahudi ilififia sana, na matumaini yao yalikoma, hayakuweza kuwamulikia hali ya siku za mbele. Kwa wengi wao, kifo kilikuwa tukio la siri. Mbele yao waliona giza tu na wasiwasi. watu walikaa tu chini wakiwa na wasiwasi bila hakika ya mambo yajayo. Walingojea kwa hamu kuu kumwona Mkombozi atakayewaletea ufumbuzi wa mambo yajayo.TVV 18.1

    Nje ya nchi ya Uyahudi kulikuwako na watu waliokuwa wakitafuta ukweli wa mambo. Kwa watu kama hao, walivuviwa Roho Mtakatifu. Maneno ya unabii yaliwaamsha; wakawa na tumaini la mambo ya mbele. Hawa walikuwa watu wa mataifa, siyo Wayahudi.TVV 18.2

    Kwa miaka mamia Maandiko Matakarifu yalitafsiriwa katika lugha ya Kiyunani (Kigiriki), ambayo ilikuwa ikizungumzwa katika dola ya Kirumi. Wayahudi walikuwa wametawanyika kila mahali, kwa kutekwa, na matumaini yao juu ya Masihi ajaye, yaliaminiwa na baadhi ya watu wa mataifa pia. Katika watu ambao waliona vibaya kwa jinsi Wayahudi walivyoiga desturi za kikafiri, walikuwa wakichunguza Maaandiko kuhusu kuja kwa Masihi kuliko walimu wa Kiisraeli.TVV 18.3

    Miongoni mwa watu waliotumaini kuwa Masihi atawaokoa toka dhambini, walichunguza kwa makini kuona asili ya mafanikio ya Wayahudi. Lakini Wayahudi walikazana tu kujitenga na mataifa mengine, wala hawakutaka kuwajulisha elimu ya Mungu, jinsi walivyoipokea wao. Unabii ulielezea kwa njia ya alama ambazo zote zilikuwa zinaelekeza kwa yule ajaye, yaani Masihi. Mafundisho lazima yatolewe kwa lugha ya kibinadamu. Kristo ajaye lazima aeleze mafundisho yaliyo dhahiri, yenye kufahamika wazi ili kupambanua makapi na ngano, ambayo yalivuruga mambo, na kuyafanya kuwa hayana maana.TVV 18.4

    Baadhi ya Wayahudi walisimama imara na kuyatunza maagizo ya Mungu kamili. Hawa waliimarisha imani yao kwa njia ya kusoma maneno yaliyosemwa na Musa, kuwa; “Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu kama mimi; msikieni katika mambo yote atakayonena nanyi.” Matendo 3:22. Walisoma jinsi Mungu atakavyomtia mafuta mtu, “ahubiri habari njema kwa wanyenyekevu, “kufunguliwa kwa; kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Isaya 61:1, 2. “Atafanya hukumu katika nchi, visiwa vitangojea sheria yake.” Isaya 42:4. Mataifa yataijilia nuru yake, na wafalme wataujilia mwanga wa kuzuka kwake.” Isaya 60:3.TVV 18.5

    Maneno ya Yakobo ya wakati akifa yaliwapa tumaini. “Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, wala mfanya sheria katika miguu yake, hata Shillo aje.” Mwanzo 49:10. Taabu ya Israeli ilishuhudia kuwa Masihi anakaribia kuja. Kulikuwa na kutazamia kwingi sana kuja kwa Mkuu atakayekuja kuusimamisha ufalme katika Israeli, naye atakuja kama Mkombozi wa taifa.TVV 19.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents