Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hakuna Mashaka wala kusitasita

  Alinena kama mwenye mamlaka. Marabi walinena kwa kusitasita, wakiwa na mashaka, na maana ya maandiko. Lakini Yesu alifundisha ukweli bila shaka yoyote. Fundisho lolote alilofundisha, alilinena kwa mamlaka.TVV 136.3

  Walakini alinena kwa juhudi na kwa moyo, si kwa magombano. Kwa kila hali, Mungu alidhihirishwa. Yesu alitaka kuvunja hali ya kupumbaza, inayowang’ang’ania watu katika mambo ya ulimwengu. Aliweka mambo ya ulimwengu kuwa, ni hafifu kulinganisha na ya milele. Lakini hakusahau umuhimu wake. Alifundisha kuwa, kufahamu mambo ya Mungu vema, humtayarisha mtu kutekeleza mambo ya dunia kwa uzuri zaidi, katika maisha ya kila siku. Akifahamu uhusiano wake na Mungu, alitambua nia mwungano wake na kila mtu katika ujamaa wa kibinadamu.TVV 136.4

  Alijua jinsi ya kunena kwa mtu mchovu, kwa wakati unaofaa. Isaya 50:4. Alikuwa na busara na jinsi ya kukutana na wenye chuki, na kuwaambia mifano itakayowavuta. Mifano yake alitumia mambo ya kila siku katika maisha. Ingawa huwa vielelezo rahisi sana, walakini huwaingia wasikilizaji wake kabisa. Ndege, maua, mbegu, mchungaji kondoo wa vielelezo hivi vyepesi, alifundisha ukweli. Na baadaye walipovikumbuka na kuviona, walikumbuka fundisho lake, au mafundisho yake.TVV 136.5

  Kristo hakuwasifusifu watu kamwe, wala kuwatukuza kwa ajili ya mambo yao mazuri. Lakini bila chuki wasikilizaji wake waliona kuwa maneno yake, kwa kweli ni ya busara, nayo yanapima ujuzi wao. Wasomi wakubwa waliburudishwa kwa maneno yake, na wasiokuwa na elimu walifaidika. Aliwafanya hata watu wa mataifa waone kuwa ujumbe wake unawahusu pia.TVV 136.6

  Hata katikati ya uhasama mkali, ulikaa katika hali ya salama. Tabia yake ya upendo, usemi wake na hali yake ya upendo, viliwavuta wote kwake, wale ambao hawakuharibiwa roho zao na hali ya kutoamini. Watu wenye dhiki na mateso walimhesabu kuwa rafiki mfadhili mkuu, nao walitaka kujua zaidi ukweli anaoufundisha. Walitamani kukaa kwenye fadhili zake siku zote.TVV 137.1

  Yesu aliziangalia nyuso za wasikilizaji wake. Alipoziona jinsi zinavyong’aa kwa kuchangamka, zilimtia nguvu, na utoshelevu mkubwa. Mishale ya ukweli ilipokuwa ikipenya katika roho za watu wapendao ubinafsi, wakigeuka kuwa wema, Mwokozi alifurahi. Macho yake yalipowaona watu, ambao walikutana naye siku zilizopita, aling’aa kwa furaha. Aliposema maneno ya ukweli kwa wenye kushikilia sanamu, yaani anasa ya dunia, hali yake ilionyesha kuwa ujumbe wake haukukubalia na watu hao. Alipoona kuwa watu wameukataa ujumbe wa amani, roho yake ilisonononeka vikubwa mno.TVV 137.2

  Katika sinagogi Yesu alipokuwa akifundisha alikomeshwa, ili amweke huru mtu aliyefungwa na Shetani, yaani mwenda wazimu aliruka kutoka katika mkutano, huku akipiga makelele na kusema: “Tuache, tuna nini nawe, Ee Yesu wa Nazareti? Je umekuja kutuangamiza? Najua kuwa wewe mtakatifu wa Mungu.” Mambo yalichafuka na kuvurugika. Watu waliangalia mambo ya mtu huyu, wakaacha mambo ya Yesu. Lakini Yesu alimkemea pepo, akisema: “Nyamaza, mtoke.” Wakati pepo alipomwangusha kati ya watu, alimtoka asimzuru.TVV 137.3

  Mtu huyu aliyesumbuliwa hivyo, mawazo yake yalikuwa yameharibiwa na Sheteni lakini alipofika kwa Yesu aliamka kutaka afunguliwe kutokana na kifungo hicho cha Shetani. Lakini pepo mchafu alishindana ili amng’ang’anie. Mtu huyu alipotaka kuomba msaada kwa Yesu, pepo mchafu alitia maneno kinywani mwake, akapiga makelele kwa masumbuko na hofu.TVV 137.4

  Mwenye pepo mchafu alifahamu kidogo kuwa alikuwa mbele ya mwenye uwezo wa kumponya, lakini alipojaribu kumsogelea yule mwenye uwezo wa kuponya, alizuiliwa na uwezo fulani, uwezo huo ukaweka maneno fulani kinywani mwake. Mashindano baina ya Shetani na yeye yalikuwa makubwa.TVV 137.5

  Pepo mchafu alitumia uwezo wake wote ili amshikilie mtu huyu. Ilionekana kuwa mtu huyu atapoteza maisha yake, katika mashindano haya na adui huyu aliyeharibu hali yake. Lakini Mwokozi aliamuru na mtu akafunguliwa. Mtu huyu alisimama katika kundi la watu, hali wakishangaa, lakini wakifurahi kwa kuponywa kwake. Hata pepo mchafu alishuhudia mamlaka ya Mwokozi. Macho ya mtu huyo yaliyokuwa yakitisha sana kuangalia, yalionekaria matulivu yakishukuru nguvu ya Yesu. Watu wakasema: “Jambo gani hili? Hili ni fundisho jipya! Kwa amri huwaamuru hata pepo wachafu nao humtii.”TVV 137.6

  Mtu huyu amekuwa ameharibiwa na anasa za dhambi naye alidhani kuwa maisha yake yatakuwa yenye furaha na sikukuu. Hakufikiri kuwa atakuwa kitisho kwa watu, na shutumu kwa jamaa yake. Alidhani kuwa maisha yake yatakuwa katika hali safi ya upuzi wa anasa. Lakini pasipokuwa na kiasi na upuzi viliyaongoza maisha yake vibaya, na Shetani akamteka. Wakati alipotaka kujiokoa katika mtego huo, hakuweza. Alikuwa ameshikiliwa katika uwezo wa mwovu. Shetani alikuwa ametawala viungo vyake vyote. Mtu huyu alipokwisha kuwa katika utawala wake, Shetani akamtendea mambo ambayo hayana huruma. Ndivyo ilivyo kwa watu wanaojiweka katika mikono ya Shetani. Mtu anayejitumbukiza katika maisha ya anasa katika maisha yake ya ujana, huishia katika hali ya wazimu.TVV 138.1

  Roho ile iliwatawala Wayahudi wasioamini, lakini kulikuwako na Yesu ambaye alikuwa mtawa. Hali ya Wayahudi wasioamini ilikuwa mbaya kuliko ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Maana wao hawakumhitaji Kristo. Kwa hiyo walikuwa katika uwezo wa Shetani zaidi.TVV 138.2

  Kuwako kwa Kristo, akifanya kazi kati ya watu, kulikuwa na juhudi kuu na msukosuko mkuu wa ufalme wa giza. Kwa vizazi na vizazi Shetani amewakandamiza watu katika masumbuko na maradhi ya namna namna. Amewatumbukiza dhambini na matatizoni. Halafu amemsingizia Mungu kuwa ndiye amesababisha hayo yote. Yesu alikuwa akiwafunulia watu tabia ya Mungu jinsi ilivyo. Alikuwa akivunja uwezo wa Shetani na kuwaweka watu huru kutokana na mambo ya Shetani. Upendo na uwezo wa mbinguni ulikuwa ukiwachangamsha watu, na mkuu wa giza alichukizwa sana. Alipinga kazi ya Kristo kwa kila hatua.TVV 138.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents