Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Watumishi halisi wanavyofundishwa

    Yesu aliwachagua wavuvi ambao siyo wasomi waliofundishwa katika shule zenye makosa na desturi za wakati huo. Walikuwa watu wenye nguvu, wanyenyekevu, wenye nia ya kufundishwa. Katika hali ya kawaida, wengi walikuwa katika shughuli zao bila kutazamia mambo makuu ya ulimwengu. Wanahitaji mtaalamu awaamshe na kuwapa mambo yatakiwayo duniani. Watu wa jinsi hiyo ndio waliitwa na Yesu wawe watendakazi pamoja naye. Wanafunzi walipotoka kwa mafundisho ya Mwokozi, walikuwa sawa na Yeye katika nia, na katika tabia.TVV 134.1

    Kazi ya juu zaidi katika kufundisha ni ile ya kuzoeza nia kutafakari mambo ya juu, inayokutanishwa na nia kwa nia, na moyo kwa moyo. Maisha huhuika kwa njia hiyo tu. Basi ilikuwa bahati gani, kwa watu hao, kukaa na Kristo miaka mitatu kila siku. Yohana alisema: “Kutokana na ukamilifu wake, tumepokea neema kwa neema.” Yohana 1:16. Maisha ya watu hawa, pamoja na kujenga tabia zao, na kazi kubwa iliyofanywa kwa ajili yao, ni kithibitisho cha vile Mungu anavyofanya kwa wote wanaokubali kufundishwa na kutii. Hakuna kikomo kwa kutumika, kwa mtu ambaye anaweka kando ubinafsi, na kumkaribisha Roho Mtakatifu afanye kazi moyoni mwake, na kuweka maisha yake wakfu kwa kazi ya Mungu. Kama watu watakubali kujiweka wakfu kwa Mungu, atawafundisha saa kwa saa wapate kufaulu. Mungu huwachukua watu jinsi walivyo, naye huwafundisha wafae kufanya kazi yake. Roho Mtakatifu akikaa ndani yao, atawarekebisha wafae kutumiwa naye. Nia inayojitoa kwa Mungu kamili, itakuzwa na kurekebishwa, halafu kutimiza matakwa ya Mungu. Tabia mbaya itatengenezwa kuwa kamili.TVV 134.2

    Ushirika wa kuendelea baina ya Yesu na wanafunzi wake, ulifanya maisha yao ya Kikristo yafanane naye katika hali zote. Atazidi kupata uwezo wa Yesu ukimwezesha kutambua hali halisi ya Kikristo. Naye atazaa matunda kwa utukufu wa Mungu. Wakristo katika maisha yao ya kawaida, watakuwa wamepata elimu ya juu sana katika shule ya Kristo. Maana wameketi chini ya mtu ambaye hakuna mtu “aliyenena kama yeye.”TVV 134.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents